Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ina lengo la Kuongoza utoaji wa elimu ya awali, msingi, sekondari, watu wazima, elimu isiyo rasmi
na mafunzo ya ufundi stadi; na kukuza utamaduni, maadili na maendeleo ya vijana. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
(i) Kuratibu usimamizi wa shule za awali, msingi, sekondari, watu wazima, wasio
elimu rasmi na mafunzo ya ufundi stadi.
(ii) Kutambua na kuratibu upangaji wa walimu katika shule za awali, msingi na
shule za sekondari katika Mkoa kwa kushirikiana na TAMISEMI.
(iii) Kuratibu utekelezaji wa viwango vya elimu na sifa za mafunzo ya ufundi stadi.
(iv) Kusimamia mitihani ya msingi na sekondari katika Mkoa kwa kushirikiana na
NECTA.
(v) Kusimamia utoaji wa mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia shuleni.
(vi)Kusimamia Mwongozo wa upatikanaji wa mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
(vii) Kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu isiyo rasmi katika Mkoa.
(viii) Kuratibu na kusimamia utambuzi wa vipaji na Maendeleo yao.
(ix) Kuanzisha na kudumisha kanzidata ya elimu na ukuzaji ujuzi wa Kikanda.
(x) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya ukaguzi wa shule.
(xi) Kuongoza mipango ya maendeleo ya utamaduni na michezo shuleni.
(xii) Kuratibu shughuli za sanaa na michezo shuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa