Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe.Sakina Jumanne Mohamed amezipongeza Halmashauri ya wilaya ya Bukombe na Mbogwe Kwa Kupata Hati Safi Miaka Mitatu Mfululizo .
Akiongoza Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani tarehe 16 Juni 2025 kujadili majibu ya hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Mhe Sakina amesema hati safi walizopata halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Mbogwe ni kutokana na ushirikiano mkubwa wa watumishi na Baraza la Madiwani kusimamia nyaraka za mapato na matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mhe. Sakina ameongeza kuwa Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hizo waongeze vyanzo vya mapato ikiwemo ujenzi wa stendi,soko na viwanda vidogo vidogo.
Mhe.Sakina Mohamed ametoa wito kwa wakaguzi wa ndani kutoa elimu na ushauri wa namna ya kujibu hoja kwa wakati na kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa nje na sio kuwakwepa wanapokuwa kwenye shughuli ya kukagua nyaraka za matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi.
Katibu Tawala Mkoa wa Geita Ndg.Mohamed Gombati amewasisitiza Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia nyaraka zote za mapato na matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi na kuongeza ufanisi wa kukusanya mapato na kuibua fursa mpya za kuongeza mapato kwenye halmashauri hizo.
Kwa Upande Wake Mthibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali Wazir Shabani,ametoa mapendezo mbalimbali kwa halmashauri ya wilaya ya bukombe na Mbogwe kuhakikisha wanazifanyia kazi hoja zao kwa wakati ili kuipunguzia kazi ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali, kuongeza mapato kutoka kwenye vyanzo vya mapato na kukusanya marejesho kutoka kwenye vikundi vya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa