Afya ndiyo Msingi wa Maendeleo kwa Taifa lolote lile. Taifa haliwezi kuwa na Maendeleo ikiwa watu wake wana afya dhaifu. Kwa kulitambua hilo, Mkoa una idadi ya Vituo vya Kutolea Huduma ya Afya 183 ambapo vituo vya serikali ni 136 (75%) na vya binafsi ni 47(25%). Kati ya hivyo hospitali ni 10, vituo vya afya 25 na zahanati 148.
Mahitaji ya mkoa ni vituo vya kutolea huduma za afya 503 hivyo upungufu ni vituo 320. Ili kukabiliana na upungufu wa vituo vya kutolea huduma za afya, tangu mwaka 2018 mkoa unaendelea na ujenzi wa jumla ya majengo 323 ya zahanati pamoja na vituo vya afya. Kati vituo 30 vipo tayari kwa ajili ya ufunguzi na kuendelea kutoa huduma na 293 vipo hatua ya mbalimbali za ukamilishaji.
Kukamilika kwa vituo vinavyojengwa, kutaongeza kiwango cha cha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kutoka asilimia 31 ya sasa hadi asilimia 96.5.Aidha, huduma za bure kwa wazee na chanjo kwa watoto chini ya mwaka mmoja na akina mama wajawazito zinatolewa katika vituo vyote 160.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa