Shule za msingi
Mkoa wa Geita una jumla ya shule za msingi 691 kati ya hizo shule 641 ni za Serikali na shule 50 zinamilikiwa na taasisi na watu binafsi. Idadi ya wanafunzi waliosajiliwa (awali hadi darasa la VII) katika shule za hizi ni 754,939 kati yao wanafunzi 73,446 wameandikishwa awali na wanafunzi 681,493 niwa darasa la kwanza hadi la saba. Uandikishaji wa awali na darasa la kwanza matarajio/maoteo yalikuwa ni kuandikisha wanafunzi 164,481. Hadi tarehe 30 Machi jumla ya wanafunzi 180,965 wa awali na darasa la kwanza wameandikishwa na wanahudhuria, hii ni sawa na asilimia 110.02 ya uandikishaji wote
Elimu ya sekondari
Mkoa una jumla ya Shule za Sekondari 155 ambapo shule 138 ni za Serikali na 17 ni za binafsi. Hata hivyo kwa mwaka huu Mkoa umesajili shule mpya 14 za kidato cha tano, kati ya hizo shule 10 ni za serikali na shule 4 ni za binafsi. Aidha, Shule hizi za serikali pamoja na za binafsi, kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita zina jumla ya wanafunzi 115,960.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa