Mkoa wa Geita una Wilaya tatu (Chato, Geita na Nyang’hwale) zenye eneo la maji ya Ziwa Victoria ambazo ndizo zinazofanya shughuli za uvuvi. Mkoa una mialo 73 (Chato 36, Geita 36, Nyangh’wale1), Chama cha Ushirika wa Wavuvi kimoja kilichopo Kikumbaitale Wilaya ya Chato na Vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali (BMUs) 56. Aidha, kati ya mialo 73 iliyopo, ni mwalo 1 tu wa Kikumbaitale (Chato) ambao umeboreshwa kwa kiwango cha kati na una sifa ya kupokea samaki kwa ajili ya viwanda vya samaki.
Katika Mkoa wa Geita kuna jumla ya wavuvi 10,001 (Chato 4,136, Geita 5,820, Nyangh’wale 45), Vyombo vya Uvuvi 2,882.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa