Leseni za madini na shughuli za madini
Shughuli za Madini zinazofanyika katika Mkoa wa Geita zimegawanyika katika makundi makuu manne (4) ambayo ni Utafiti wa Madini, Uchimbaji wa Madini (Mkubwa, wa Kati na uchimbaji mdogo), Shughuli za uchenjuaji Madini na Biashara ya Madini.
Mkoa wa Geita una jumla ya leseni 2 za uchimbaji mkubwa (Special Mining Licences - SMLs), ambazo ni leseni Na. SML 45/1999 inayomilikiwa na Kampuni ya GGML na LESENI Na. 04/1992 inayomilikiwa na Kampuni ya Backreef Gold Mine Ltd. Aidha Mkoa wa Geita una jumla ya leseni 25 za uchimbaji wa Kati (Mining Licences - MLs), leseni 1574 za uchimbaji mdogo (Primary Mining Licences - PMLs) na jumla ya leseni 215 za Utafiti mkubwa wa Madini (Prospecting Licences -PLs) zilizotolewa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa. Aidha jumla ya mitambo ya Uchenuaji – Elution Plants - 38, VAT Leaching Plants - 362 na Mitambo ya CIP - 10 na CIL - 1.
Biashara ya madini
Mkoa wa Geita una Soko Kuu (Mineral House) moja (1) lililoanzishwa rasmi tarehe 17 Machi, 2019 lenye jumla ya wafanyabiashara wakubwa wa Madini (Dealers) 37 na jumla ya Masoko Madogo (Buying Stations) nane (8) yenye jumla ya wafanyabiashara wadogo (Brokers) 67, yaliyoanzishwa katika nyakati tofauti kwenye wilaya za Mbogwe -1, Bukombe -1 Chato -1, Nyang’hwale -1 na Geita – 4. Uanzishwaji wa Masoko ya Madini umekuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha biashara ya Madini na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa