Mkoa wa Geita ni miongoni mwa Mikoa ya kanda ya Ziwa yenye vivutio vingi vya utalii. Pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii pia ndio lango kuu la kuingilia kufikia vivutio vya utalii kwa Mikoa ya Jirani kama vile Kagera na Kigoma. Uwepo wa Hifadhi tatu za Taifa kwa maana ya Kisiwa cha Rubondo, Burigi-Chato na Kigosi/Moyowosi ni vivutio vya utalii ambavyo utaona wanyama wa nchi kavu na majini. Vile vile kuna fukwe nzuri za kuvutia katika Wilaya ya Chato ambazo zinafaa kwa kupunzika kwa watalii mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa