Vipaumbele vya mkoa ni sita ambavyo ni Uboreshaji wa shughuli za uchumi, biashara na uzalishaji utokanao na viwanda, Ujenzi wa miundombinu na uimarishaji wa huduma za jamii na utawala, Kuimarisha ukusanyaji na udhibiti wa Mapato ya Ndani, Kuboresha takwimu kwa ajili ya shughuli za Maendeleo, Kuwa na Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi na utunzaji wa mazingira na Kuimarisha utawala bora. Ili kuvitekeleza viapumbel hivi Mkoa pamoja na Halmashauri zake umetekeleza miradi mbalimbali kama ifuatavyo: -
Ujenzi wa Hospitali Mbili za Wilaya ya Geita, Upanuzi wa hospitali ya Wilaya Chato, Ujenzi wa kituo cha Afya Chato, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Mbogwe, Ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale, Ujenzi na Ukamilishaji wa zahahanti 351 na Vituo vya Afya 17 katika Mkoa, Ujenzi wa Hospital ya Mkoa wa Geita, Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya Mbogwe na Nyang’hwale, Miradi ya Maji, Mradi wa Machinjio ya Kisasa, Mradi wa Ujenzi wa soko Geita Mjini, Mradi wa Ujenzi wa soko Geita Mjini, Ujenzi wa soko la Katundu, Ujenzi wa Jengo la Utawala eneo la Kituo cha Uwekezaji (Special Economic Zone- SEZ) Halmashauri ya Mji Geita, Ujenzi wa kiwanda cha Kuchakata Asali Bukombe, Ujenzi wa soko la kisasa la Katoro
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa