BALOZI WA JAPAN AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA NA KUSINDIKA ALIZETI WILAYANI CHATO
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida amezindua kiwanda Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha Kusafisha mafuta ya Alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double Refining Factory) Wilayani Chato chenye uwezo wa kuzalisha lita 700 kwa siku.
Kukamilika kwa mradi huo kutapelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la Alizeti na kuongeza kipato kwa wakulima wanaolima zao hilo.
Kabla ya kiwanda hicho chama cha ushirika cha AMCOS kilikuwa kikitumia teknologia ya chini katika shughuli zake za kuchakata na kusindika Ali zeti.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua kiwanda hicho balozi Yoshida amasema kuwa Serikali yake itaendelea kusaidiana na Serikali ya Tanzania katika suala la maendeleo ili kuhakikisha nchii inapiga hatua kubwa.Aidha,Dkt.Medard Kalemeni (Mb) na Naibu Waziri wa Madini amemuomba balozi huyo kusaidia ata katika ujenzi wa Viwanda vya kutengeneza magari. Kiwanda hicho kilijengwa kwa shilingi milioni 100 fedha ambazo zilitolewa na Serikali ya Japan.
Katika hatua nyingine Balozi Yoshida ametembelea ujenzi wa soko la kimataifa la Samaki lililopo kijiji cha Kasenda- Muganza Wilayani Chato ili kujionea hatua ya utekelezaji wake ambao Japan inafadhili kwa gharama ya shilingi milioni 320.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa