Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita imeendelea kutekeleza jukumu chini ya ofisi ya kamishna wa kazi kwa kuunda mabaraza ya wafanyakazi nchini na kuketi vikao vya kisheria ikiwa ni namna ya ushirikishwaji wa wafanyakazi sehemu za kazi.
Utekelezaji wa jukumu hilo umeendelea kuthibitika leo Juni 2, 2022 baada ya kuketi kwa kikao cha pili kwa mwaka wa fedha 2020/2021katika ukumbi mdogo wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.
Akiongea wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi sekretarieti ya mkoa wa Geita, Bw. Herman Matemu ambaye ni kaimu katibu tawala mkoa na mwenyekiti wa kikao hicho amesema, ni muhimu wajumbe wote kutoa michango yao katika kuboresha mambo mbalimbali yahusuyo watumishi.
Amesema, “hiki ni kikao cha pili na cha mwisho kwa mwaka huu wa fedha kama ilivyo taratibu kuketi vikao viwili kwa mwaka, hivyo niwaombe tuwe makini kusikiliza na kuchangia ili michango yetu iwe na tija”
Awali, katibu wa baraza msaidizi Bi.Sarah Mwangole ambaye pia ni mwanasheria ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita amesema, ni muhimu kwa wajumbe kuzingatia yale yatakayotokana na kikao hicho ili kuwa na mwelekeo sahihi kwa malengo yaliyowekwa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe kutoka sekretarieti ya mkoa pamoja na wa wilaya za mkoa wa Geita wakiwemo kutoka vyama vya wafanyakazi
Boazi Mazigo
Ag.HGCU
Juni 24, 2022
GEITA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa