Na Boazi Mazigo- Geita RS
Wilaya ya Bukombe imepongezwa kufuatia utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, hali iliyopelekea viongozi mbalimbali kutoa wito kwa wataalam kuendelea kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ili kupata matokeo chanya.
Hayo yalielezwa Agosti 22, 2023 baada ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa Geita kupitia Miradi mbalimbali yenye thamani ya jumla ya shs. 2,974,632,338 katika wilaya hiyo ambapo wajumbe wote kwa pamoja wameeleza kuridhika na usimamizi, ubora na thamani ya matumizi ya fedha.
Akiongea kwa nyakati tofauti akiwa kwenye miradi ya sekta ya elimu, afya, maji na barabara, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwenyekiti CCM Mkoa Geita Nicholaus Kasendamila alisema "niwapongeze sana Bukombe kwa viwango vya ubora, usimamizi na utekelezaji miradi mbalimbali. Nimpongeze pia Mkuu wa Wilaya Mhe.Said Nkumba, Mbunge Dkt.Doto Biteko na Viongozi wengine wote kwa ushirikiano hadi kufanikisha kazi hizi"
Kasendamila aliongeza kuwa, ni vyema kila mahala wanapojiwekea utaratibu ufuatwe ili uweze kuwasaidia vinginevyo, ni ngumu kufikia malengo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Bukombe Mhe.Said Nkumba kwaniaba ya wanabukombe aliwashukuru na kuwapongeza viongozi wenzake kwa kufanikisha utekelezaji mzuri wa miradi, huku akisisitiza kuwa, ubora wa miradi huo unatokana na utaratibu waliojiwekea wa ununuzi wa baadhi ya vifaa kwa pamoja hali inayopelekea miradi yote kuonekana ya ubora unaofanana na kusisitiza kuwa wataendelea kuusimamia kwani umeonesha tija ya utekelezaji
Kwaniaba ya mkuu wa mkoa geita, Mhe.Cornel Magembe ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya geita, naye aliungana na viongozi wengine kuipongeza Bukombe kwa jinsi ilivyojidhatiti kuwatumikia wananchi wake kupitia usimamizi wa miradi mbalimbali wilayani humo.
Naye Bi.Neema Mbuliga mkazi wa Mtakuja alisema, "tunaishukuru sana serikali yetu pendwa, tunamshukuru Sana Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, na mbunge wetu Mhe.Dkt.Doto Biteko pamoja na viomgozi wote wilayani hapa kwa kupigania maendeleo hadi kutuletea miradi mbalimbali ukiwemo huu wa maji kupitia RUWASA. Tunaamini mahusiano ya familia zetu yataimarika sasa pamoja na afya zetu lakini pia mmetutua ndoo kichwani"
Mwisho, kamati hiyo itaendelea na ziara yake Angostura 23, 2023 katika wilaya ya Mbogwe na kisha wilaya nyingine zote za mkoa wa Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa