Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt.Ashatu Kijaji amezindua zoezi la Chanjo ya Homa ya Mapafu kwa Ng'ombe Mkoani Geita Pamoja na Zoezi la Uvikwaji wa Hereni kwa Ng'ombe tarehe 6 Julai 2025.
Uzinduzi huo umefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Chato na Bukombe lengo likiwa ni Kupandisha thamani ya Mifugo na Kuachana na utaratibu wa Kuwagonga mihuri ya moto kwenye ngozi.
Dkt. Kijaji ametoa wito kwa wafugaji kujitokeza kupeleka mifugo yao kupata chanjo ili mifugo hiyo iwe na thamani na kuweza kuuzwa nje ya Nchi. Pia ameongeza kuwa uchanjaji wa mifugo utakuwa ni bure ambapo chanjo zinazotolewa ni pamoja na chanjo ya homa ya mapafu,Sotoka kwa mbuzi,chanjo kwa London na chanjo ya kideli kwa kuku na bata.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigela, amesema mkoa wa Geita una takribani ng'ombe milioni moja na laki mbili pamoja na wataalam wa mifugo wa kutosha ambao wapo kwa ajili ya kutoa huduma ya chanjo nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuongeza thamani ya mifugo mkoani Geita.
Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Mifugo Mkoa wa Geita Dr.Sosthenes Nkombe,amesema zoezi la uvikwaji wa hereni kwa ng'ombe litasaidia kufanya usajili wa kidijitali wa kujua idadi ya ng'ombe anazomiliki mfugaji kwa kuzingatia umri,jinsia,rangi na picha ya ng'ombe kwa kutumia namba iliyoandikwa kwenye hereni.
Pia zoezi la uvikwaji wa Hereni kwa Ng'ombe itaondoa changamoto ya wezi wa mifugo.
Wafugaji wa Mkoa wa Geita wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwawezesha kupata chanjo hususani ya homa ya mapafu kwa ng'ombe ambayo iliwatesa kwa muda mrefu.
Kampeni ya chanjo ya Ng'ombe na Uvikwaji wa Hereni inaongozwa na kauli mbiu isemayo"Ufugaji Maisha Yetu"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa