Katibu mkuu wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Allan Kijazi ameuhakikishia uongozi wa mkoa wa geita kuwa, wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwao ili kutatua changamoto mbalimbali za ardhi zinazoukabili mkoa huo ili kwa pamoja kuwaondolea wananchi kero na adha zitokanazo na migogoro ya ardhi.
Hayo yamesemwa leo januari 27, 2022 wakati katibu mkuu huyo alipowasili ofisi ya mkuu wa mkoa wa geita katika ziara yake ya kikazi kukutana na watendaji wa ardhi wa mkoa wa Geita huku akisisitiza ofisi za halmashauri kushirikiana katika ukusanya maduhuli ya serikali kupitia makusanyo yatokanayo na ardhi.
“kwanza nikupongeze Mhe.Senyamule kwa kazi nzuri, lakini nikuahidi ushirikiano kutoka kwenye wizara ya ardhi katika kutatua changamoto mbalimbali za ardhi, lengo kuu ikiwa ni kuwasaidia wananchi kuondokana na migogoro mbalimbali ya ardhi, hivyo hili ni jukumu letu sote. Vilevile niombe kupitia ofisi hii kuwahimiza halmashauri za mkoa huu kuendelea kushirikiana na watumishi wa ardhi kukusanya maduhuli ya serikali ili kwa pamoja tuijenge nchi na kujiletea maendeleo”, alisema Dkt.Kijazi
Naye mkuu wa mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Senyamule amemshukuru Dkt.Kijazi kwa kufika ofisini kwake kisha kumueleza changamoto za ardhi mbalimbali zinazoukabili mkoa wa geita huku akieleza namna mkoa ulivyojizatiti kutunza mazingira kwa manufaa ya maisha ya sasa na baadaye kwa mstakabari wa taifa la Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa