Mkoa wa Geita umezindua Operesheni Anwani ya Makazi yenye kaulimbiu “Mfumo wa Anwani za Makazi kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi” yenye lengo la kuwezesha ufanisi wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kuanza mwezi Agosti 2022, lakini pia ikiwa ni njia ya kurahisisha ufikiwaji wa wanachi kwa urahisi hivyo kuchangia kasi ya maendeleo.
Akiongea na watendaji pamoja na wananchi wa Nyankumbu mjini Geita, mkuu wa mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Senyamule amewataka watendaji kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo kwa kasi na kwa ufanisi tena kwa kutumia rasilimali zilizopo ili kufanikisha zoezi huku akisisitiza kuwa zoezi hilo kimkoa likamilike kufikia tarehe 15 Aprili, 2022.
“kwanza tumshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu wa kuanza kutekeleza jambo hili kwani kwa miaka yote tumekuwa tukifanya sensa ya watu bila makazi, lakini kwa hatua hii tutasonga mbele. Pia, niwaombe wananchi kuwa tayari kwani baada ya uzinduzi huu kutakuwa na wiki moja ya kutoa elimu, kisha kuchagua majina na kuyabandika kwenye Mitaa. Muhimu, ni kuhakikisha wakurugenzi mnatumia rasilimali zilizopo ili kufanikisha zoezi hili ndani ya miezi miwili kutoka tarehe ya leo”. Alisema Mhe.Senyamule kisha kuzindua kwa kukata utepe kwenye nyumba ya Bi. Edina Kabyemela, Mwananchi wa Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu-Halmashauri ya Mji Geita.
Awali, Mhe.Senyamule aligawa mfano wa vibao vyenye namba zitakazotumika kuwekwa kwenye kuta za nyumba kwa Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Geita, ishara ya kuanza utekelezaji wa zoezi hilo kwenye halmashauri wanazozisimamia, zoezi lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa EPZA-Mjini Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa