• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

“HAMTOJUTIA KUWEKEZA GEITA”, Asema RC Geita kwa Bodi ya Wadhamini PSSSF

Posted on: April 9th, 2019

Geita umeendelea kuwa mkoa unaovutia uwekezaji huku ukiweka mazingira rafiki na wezeshi yasiyo na urasimu wala rushwa kwa wawekezaji wote wenye nia njema ya kuwekeza, jambo linalopelekea ugeni wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF kupiga hodi Geita kwa lengo la kuwekeza kwenye ardhi na kupokelewa na mwenyeji Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Aprili 8, 2019 ofisini kwake.

Akizungumza na wajumbe wanaounda bodi hiyo, Mhandisi Gabriel amewaambia kuwa, Geita ni mkoa wa utajiri na wa kimkakati huku akiwaeleza jinsi unavyozalisha dhahabu kwa zaidi ya asilimia sabini, vilevile mkoa unaokwenda kufunguka katika sekta ya utalii kupitia Biharamulo, Burigi na Kimisi na kuwaibia siri ya mafanikio aliyoyapata na anayoendelea kuyapata katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile inayotumia fedha zinazotokana na mapato ya dhahabu.

“niwakaribishe sana kuwekeza mkoani hapa, hamtojutia. Nyumba za Kisasa za kupanga (apartment) na Hoteli ni miongoni mwa mahitaji makubwa kwa sasa mkoani hapa. Sisi kama serikali kazi yetu ni kuhakikisha tunaweka mazingira wezeshi ili mnapowekeza mpate faida, hakika mtaongeza imani kwa wateja wenu kwakuwa mtakuwa na hakika ya kuzalisha faida. Hatutaki kama mkoa kutegemea dhahabu pekee ndiyo sababu tunajipanga kukuza uchumi kwa kuweka miradi ya kimkakati, kuimarisha utalii kwani tumeamua na fedha ya kufanya hayo ipo”, alisema Mhandisi Gabriel.

Baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Mhandisi Gabriel aliwapitisha wajumbe hao kujionea soko kuu la dhahabu geita ikiwa masoko mengine nane yataanzishwa hivi karibuni, akawaonesha uwekezaji unaotokana na mapato ya fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) kutoka Mgodi wa Dhahabu Geita GGM huku akiwaambia , “sifanyi miujiza, nimezuia wezi kwenye miradi ndiyo maana nimefanikisha haya”.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Mussa Iyombe amemueleza mkuu huyo wa mkoa kuwa, wapo mkoani geita kuona eneo linalomilikiwa na PSSSF ili kujua ni kwa namna gani linawekezwa kisha kumshukuru mhandisi Gabriel kwa namna alivyowapokea na kuwakaribisha kuwekeza akiahidi kuyafanyia kazi mawazo waliyopewa akisema, “tumefurahia mawazo yako, tuna ahidi kuwa karibu nawe katika kufanikisha miradi tutakayoitekeleza Geita”

Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa