katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa utoaji huduma kwa wananchi, watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Sekretarieti ya Mkoa wa Geita wameketi kikao, kisha kuja na mpango wa kuwa na mkataba utakaoainisha mambo yatakayoiongoza idara kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi kwa wakati ili kuwaepushia kero mbalimbali wanapopokea huduma, Kikao kilichofanyika tarehe 05.10.2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali Watu na Mkuu wa Idara hiyo Bw.Herman Matemu amesema, lengo la kikao hicho cha kila mwisho wa mwezi ni kujadili na kuja na suluhisho la changamoto katika maeneo mbalimbali ya utendaji, ikiwa ni katika kuweka mazingira mazuri kwa watumishi kuwawezesha kutoa huduma katika nzuri kwa wananchi kisha akawapongeza kwa mahudhurio mazuri ya kikao ilihali wakiwa na majukumu mengi ya kutekeleza.
Amesema,“tutakuwa na mkataba wa huduma kwa mteja ambao utatuongoza katika kumhudumia mwananchi na ni imani yangu kuwa tutakayokubaliana tutayatekeleza ili kuleta matokeo chanya”.
Kwa upande wake Afisa Tawala Mkuu, Bw. Masoud Biteyamanga amewakumbusha watumishi juu ya kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni (STK) kwakuwa ndiyo dira ya mtumishi awapo kazini.
Naye Afisa Tawala Bi. Beatrice Masanja amewakumbusha watumishi juu ya kuwa na mahusiano mazuri na ushirikiano ambapo kwavyo ni rahisi kuonesha matokeo kwani bila mahusiano mazuri kazini ni vigumu kufikia malengo idara iliyojipangia.
Mwisho, watumishi wengine walitoa maoni yao wakisisitiza suala la heshima baina ya watumishi pamoja na kusaidiana kwa yeyote atakayekwama katika suala zima la utekelezaji wa majukumu ya kila siku, lengo ikiwa ni kufanikiwa.
Miongoni mwa watumishi wa idara hiyo waliohudhuria ni pamoja na Madereva, Watunza Kumbukumbu, Wahudumu, Makatibu Muhtasi pamoja na Afisa Habari.
.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa