VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI MKOANI GEITA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA / VIONGOZI WENYE DHAMANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mkoani Geita kushirikiana na mamlaka au viongozi husika wa wafanyakazi wenye dhamana ya kutafuta majawabu ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi.
Mkuu wa Mkoa amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo kimkoa imefanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala mjini Geita na kushirikisha watumishi mbalimbali wa Serikali na Sekta binafsi."Nimesikiliza risala yenu masuala mliyowasilisha ni ya msingi sana kwa maslahi na ustawi wa wafanyakazi wa Mkoa wetu, changamoto na kero hizi naamini baadhi zipo ndani ya uwezo wenu ninyi kama chama cha wafanya kazi katika kuzitafutia majawabu.Vyama vya wafanyakazi vipo kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa Umma, na viongozi wakekwa kushirikiana na waajiri mnayo dhamana kubwa ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi".
Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa waajiri wote katika Mkoa wa Geita kuhakikisha wanafanya rejea ya masuala mbalimbali ya kiutumishi kuhusu haki na maslahi ya wafanyakazi na kuyafanyia kazi kikamilifu ili kuondoa changamoto na kero zisizo na ulazima. Pia amewataka watumishi kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo na kutatua kero zao kwa wakati na kujiepusha kabisa na vitendo vya kutoa na kupokea Rushwa
Magesa Jumapili (Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa