Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ameshiriki katika kazi za jamii kwa kufyatua matofali ya saruji (block) kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Kamena iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akiwa katika kituo hicho, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kufanya kazi bila malipo na kuwataka kuendelea kujitolea michango yao ya hali na mali ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Geita kwa kuboresha miundombinu ya Elimu na Afya. Akiwa katika Kata hiyo, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amesisitiza masuala ya wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili wakaelimike na baadae walisaidie taifa.
Amezungumzia pia masuala ya mimba na ndoa za utotoni ambapo amesisitiza kwa kusema “serikali haitafumbia macho mtu atayehusika na matendo haya”.
Sambamba na hayo, Mkuu wa Mkoa amesisitiza suala la mshikamano katikautekelezaji wa miradi mbalimbali ya jamii.
Katika ujenzi huo, wananchi wamejitolea kwa kuchangia mawe, mchanga, ufundi na mali wakati Halmashauri ya Wilaya imeunga mkono juhudi hizi kwa kuchangia Shilingi Milioni Thelathini ( Tshs. 30,000,000/=) ambazo zitasaidia kukamilisha ujenzi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa