MAAFISA KILIMO NA MIFUGO WATAKIWA KUWA CHACHU YA UCHUMI WA VIWANDA MKOANI GEITA
Maafisa kilimo na Mifugo Mkoani Geita wametakiwa kuwa chachu ya kufikia Uchumi wa Kati na Viwanda Mkoa wa Geita kwa kuboresha shughuli za kilimo na mifugo ili kuongeza tija.
Akizungumza na watendaji hao wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na kituo cha utafiti wa Mbegu cha Maluku Mkoani Kagera, Mhe. Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema kila siku lazima kuwe na jitihada za kubadilisha mienendo katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kuleta tija ili kutupekeka katika uchumi wa viwanda na baadae uchumi wa kati kwa kutumia rasilimali zilizo katika shughuli za kilimo, mifugo. Ametoa wito wa kufanyia kazi yale yote waliojifunza ili yalete tija kwa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Geita.
Aidha, katika kikao hicho katibu Tawala wa Mkoa wa Geita ndugu Selestine Gesimba amesema kuwa serikali ya Mkoa inafanya jitihada za kuweka utaratibu wa kuendesha shuguli za kilimo na ufugaji katika kila Wilaya zote za Mkoa wa Geita kwa kuazisha mashamba darasa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uzalishaji na kipato cha mwananchi.
Katika kikao hicho wataalamu hao walipata fursa ya kutembelea shamba darasa ambalo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa lenye kilimo cha Alizeti, Maharage,Mahindi, Mtama na bwawa la ufugaji wa samaki lenye vifaranga 120. Shamba hilo linalenga kutoa elimu kwa wananchi ili wajue mbinu za kuendesha kilimo bora chenye tija kwa wakulima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa