Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Mhe.Grace Kingalame ametoa wito kwa Watumishi wa Umma Katika Mkoa wa Geita kuendeleza desturi ya kufanya mabonanza ya michezo kwa lengo la kuboresha afya zao na kuimarisha mahusiano.
Mhe. Kingalame ametoa wito huo alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati wa ufungaji rasmi wa Bonanza la watumishi wa Umma Mkoani Geita lililofanyika Machi 29, 2025 katika Viwanja Vya Shule ya Msingi Waja Geita mjini.
Mhe.Grace Kingalame ameongeza kuwa Bonanza hili ni Kwa ajili ya burudani,mazoezi,kudumisha ushirikiano na mshikamano na kujadiliana mambo muhimu yanayohusu utumishi wa Umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kila wakati
Mhe. Kingalame amewakumbusha watumishi hao kutambua kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan inatambua Mchango wa Watumishi wa Umma Kwenye kuleta maendeleo na inahakikisha watumishi wa Umma wanakuwa mazingira bora ya kazi na kuboresha maslahi bora.
Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa Wa Geita Dkt.Omari Sukari amesema Bonanza hili Limetimiza Muongozo wa Serikali wa Kuendelea Kupambana na Magonjwa Sugu yasiyoambukiza na kuepuka ugonjwa wa Ukimwi Maeneo ya Kazi pia Bonanza hili linaongeza upendo,umoja na mshikamano wa Watumishi wa Umma Mkoani Geita.
Kwa Upande Wake Afisa Michezo Mkoa wa Geita,Bahati Rodgers amesema Bonanza hili ni La Kwanza,kwa Mwaka 2025 Kutakuwa na Mabonanza manne ambayo yatafanyika Kila Baada ya miezi mitatu.
Washindi Walioibuka na ushindi wa Vikombe kwenye Bonanza katika mchezo wa Mpira wa Pete ni Hospitali ya Manispaa Geita, mchezo WAVU ni Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mchezo wa kuvuta KAMBA kwa wanawake ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita, kwa Wanaume ni Tume ya Madini,mchezo wa mpira wa KIKAPU ni Hospitali ya Mkoa wa Geita ,MPIRA WA MIGUU mshindi ni Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Washindi wa Mchezo wa Riadha, Karata ,Bao, Kisahani,Kukimbia na Yai,Kurusha Mkuki ,Kukimbia na Magunia Walipewa Zawadi za Medali.
Zawadi ya Mchezaji bora mpira wa miguu Mshindi ni Faller Mabije kutokea GEUWASA
Zawadi ya Mfungaji bora mpira wa miguu mshindi ni Elneo Nyongole kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa