Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amefungua kikao cha uhabarishaji na kutambulisha Mradi wa Afya Kwanza unaoratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Management Development for Health (MDH), kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa tarehe 06.02.2019.
Akifungua kikao hicho, Mhandisi Gabriel ameanza kwa kuwashukuru na kuwakaribisha MDH ambao wamekuja kwa lengo la kuutambulisha mradi wa Afya Kwanza na kwamba mkoa utaendelea kutoa ushirikiano huku akisisitiza juu ya viongozi kutambua kuwa wana mustakabali wa afya ya wanaGeita, hivyo kutoa maoni yao wakati wa majadiliano kutaleta matokeo chanya.
Amesema, “Kipekee, naomba kutumia nafasi hii kuwashukuru Shirika la MDH kupitia PEPFAR, Shirika la ICAP, Shirika la Intrahealth na wadau wengine wa Mkoa kwa michango yenu ya rasilimali fedha na utaalamu katika kuboresha huduma hapa nchini. Nawakaribisha sana, lakini pia nishukuru kwa jitihada na mikakati mliyonayo ya kuhakikisha jamii ya mkoa wetu inakuwa na afya njema, zaidi katika mkakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo tunatakiwa kuendelea kufanya vizuri kwenye 90, 90, 90 pamoja na taarifa nzuri niliyoipata kuwa zaidi ya asilimia 90% ya vijidudu vimefubazwa” kisha kufungua kikao na kuomba viongozi kutambua yakwamba wana dhamana kubwa ya kuhakikisha afya ya wananchi inakuwa imara.
Akiutambulisha Mradi wa Afya Kwanza, Meneja Mkuu wa Shirika la MDH Tanzania Bw.Emilian Busara amesema kuwa watakuwa Geita kwa miaka mitano na kwa utaratibu wa kusaini mkataba kila mwaka. Ameendelea kusema kuwa, shirika hilo linayo malengo yake ikiwemo ya kuhakikisha 90, 90, 90 zinafikiwa yani upimaji, kuanzisha tiba kwa waliobainika kuishi na VVU, uimarishaji wa utoaji wa huduma bora za tiba na matunzo (CTC) kwenye vituo vya afya, vilevile kuimarisha mifumo ya utoaji takwimu za afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa