Mkoa wa geita wazindua utoaji wa chanjo mpya ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana waliotimiza umri wa miaka 14
Mkoa wa Geita umezindua rasmi utoaji wa Chanjo Mpya ya Kujikinga na Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana waliotimiza umri wa miaka 14 ambapo uzinduzi huo umefanywa na Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita.
Akiwahutubia wananchi wa mji wa Geita na wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi huo Mhandisi Robert Gabriel amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vilivyopangwa ili wapate chanjo hii muhimu kwa afya ya akina mama kwa kuwa inatolewa bure kwani serikali imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha inalipia chanjo hii ili wananchi wapate huduma.
Aidha, amewataka wanafunzi kuacha tabia ya kufanya ngono wakiwa na umri mdogo kwa kuwa vitendo hivyo vinahusika katika kusambaza ugonjwa huo.Vile vile amewataka kwenda kupima katika vituo vya afya na Hospitali ili kujua afya zao.
Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi imezinduliwa mjini Geita na itatolewa katika Wilaya zote tano za Mkoa wa Geita katika vituo mbalimbali vya afya na Zahanati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa