Zaidi ya Wananchi elfu 43 wa Kata ya Nkome na maeneo ya jirani watanufaika na maboresho ya huduma za afya zitakazotolewa baada ya upanuzi wa Zahanati ya Kata hiyo kuwa Kituo cha Afya kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2024.
Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Nkome, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Ndugu. Godfrey Eliakimu Mnzava amesema kuwa nia ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha Sekta ya Afya inaboreshwa ili wananchi waweze kuhudumiwa katika viwango vinavyokubalika.
Ndg. Godfrey Mnzava ameongeza kuwa ujenzi wa majengo matatu ya Maabara, Wodi ya wazazi na jengo la wagonjwa wa nje kutatoa fursa kwa wagonjwa watakaokwenda kupata huduma kuwa na eneo kubwa lisilowabana, kadhalika na watoa huduma kupata nafasi itakayowatosha kuwahudumia wagonjwa wanaofika kituoni kwa ajili ya huduma.
Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Mhe. Joseph Kasheku Msukuma ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgodi wa Dhahabu Geita kwa kuiwezesha Kata ya Nkome na kuweka kumbukumbu ambayo haitafutika katika vichwa vya wananchi wa Nkome kutokana na ongezeko la majengo katika Kituo cha Afya Nkome.
Mhe. Msukuma ameongeza kuwa Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 umefanyika chachu kwa viongozi wa Serikali katika Wilaya ya Geita na wananchi [J1] wa Kata ya Nkome kuona umuhimu wa upanuzi wa Zahanati ya Kata kwenda kuwa kituo cha Afya ili kuongeza huduma ambazo awali zilikuwa zikitolewa nje ya Kata hiyo na kuwalazimu wananchi hususan wanawake, watoto na wazee kufuata huduma hizo mbali pale inapohitajika.
Mwenge wa Uhuru 2024 umehitimisha ziara yake katika Mkoa wa Geita ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo umekimbia umbali wa kilomita 44.1 na kukagua, kutembelea, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 11 yenye gharama ya Shilingi Bilioni 2.8
[J1] e
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa