Mhe. Hussein Bashe Naibu waziri wa Kilimo ameziagiza Taasisi zilizo chini ya Wizara yake zinazoshughulika na huduma za kimaabara kupunguza gharama za huduma hizo ili kuhakikisha Upimaji wa afya ya udongo kwa Wakulima inakua ni huduma na sio biashara kwani itawasaidia wananchi kutambua afya ya udongo kwa mazoa wanayolima na kujua watumie mbolea ya aina gani.
Mhe. Bashe ameyasema hayo jana Jumatatu, Agosti 08, 2020 wakati akifungua Rasmi maonesho ya Kilimo na Sherehe za nane nane kwenye Viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza ambapo Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera wananakutana hapo kwa juma zima kukamilishamaonesho kwa Kanda ya Ziwa Magharibi.
Aidha, Mhe. Bashe amewasihi viongozi wa Mikoa na wilaya nchini kuhakikisha wanawalea Wakulima kwa kuwatafutia Masoko ya bidhaa na Mazao yao ili kuwaongezea kipato kwa mmoja mmoja na kukuza Uchumi.
Akitoa salamu, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel amewasihi wananchi waliofika kwenye maonesho hayo na wataoendelea kufika kujifunza kwa kina yatolewayo ili nao wakawaambie Wakulima majumbani wataporudi kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupeleka ujumbe kwa haraka zaidi kwa wananchi.
Vile ile Mkuu wa Mkoa wa Geita ametambulisha maonesho ya Teknolojia ya madini yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Geita ifikapo mwezi watisa mwaka huu kuanzia tarehe 17 hadi 27. Amewasihi wananchi Kuhudhuria kwa wingi bila kukosa kwani ni fursa ya kujifunza Teknolojia ya madini ambapo maonesho hayo yanafanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Wakati huo huo, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho kwenye iwanja hivyo ambapo amefurahisha na uthubutu wa makundi mbalimbali waliojitokeza kuonesha bidhaa zao na ipando ya Mazao mbalimbali viwanjani apo.
Aidha, mku wa Mkoa amefika kwenye banda la Halmashauri nya wilaya ya Bukombe ambapo amekutana na kikundi cha Bora Kilimo Biashara wanaojishughulisha na uchakataji wa Mazao ya Nafaka mabapo amewapongeza kwa kazi nzuri ya ujasiriamali nao kwa kupitia msemaji wao bwana Wilson Mola walimwonesha furaha yao kwa kuishukuru Halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa kuwakopesha Fedha Milioni 36 ambazo zimesaidia sana kukuza biashara yao.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita amepata fursa ya kuonana na vikundi mbalimbali walio na bidhaa bora zsana kwenye mabanda ya Halmashauri za Chato, Mbogwe na Geita na Mji wa Geita ambapo pamoja na kunywa Mvinyo utokanao na Matunda ya Mananasi vilevile alipata fursa ya kunywa juice nzuri inayotengenezwa kwa kutumia viazi lishe.
Maonesho ya Kilimo na Sherehe za nane nane mwaka 2020 yenye Kauli mbiu; Kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na uvui, chagua viongozi bora 2020 yamefanyika Kitaifa kwenye kanda ya Ziwa Mashariki huko Mkoani Simiyu kwenye viwanja vya Nyakabindi ambapo yamefunguliwa Rasmi Agosti 01, 2020 na Mhe. Samia Suluhu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo yatahitimishwa ifikapo Agosti 08, 2020.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa