Katika kuthibitisha kaulimbiu ya Benki ya NMB “Karibu Yako”, Benki hiyo imefanikiwa kufungua tawi la 229 katika Mji wa Masumbwe Wilayani Mbogwe, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi.
Akiongea wakati wa akifungua Tawi hilo Aprili 25, 2019, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameelezwa kufurahishwa na uamuzi wa Benki hiyo kuamua kuwekeza katika Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita hususan mji wa kibiashara Masumbwe.
Mhandisi Gabriel amesema,“nawapongeza sana NMB kwa kuchagua kuja Geita, hamjakosea, mmefanya uamuzi sahihi. Pia nipongeze hatua yenu kuthibitisha kauli yenu isemayo “karibu yako” kwakuwa nimeelezwa kuwa awali wateja wenu walitembea umbali wa kilomita 50 kuifikia huduma yenu, hongereni sana”
Hakuishia hapo, Mhandisi Gabriel aliwahimiza wananchi kupenda kuhifadhi fedha zao kwenye Benki kwa usalama zaidi kwakuwa ulimwengu umebadilika. Amewakumbusha wanananchi juu ya matumizi mazuri ya fedha na kuweka akiba akisema “usikope fedha ili kuweka heshima baa”, vilevile kujitahidi kurudisha mikopo wanayowezeshwa ili taasisi iweze kuendelea na kuwahimiza viongozi wa wilaya hiyo kuleta mpango kabambe wa upangaji mji ili kukuza miji kwa kuipanga na kuuza ardhi, kisha akakata utepe na kuweka jiwe la ufunguzi na huduma zikaanza rasmi.
Akitoa taarifa kabla ya mgeni rasmi kuongea, Donatus Richard, Mkuu wa Kitengo cha Biashara NMB, ametaja mafanikio kedekede ikiwemo Benki hiyo kuwa na mashine za kuchukulia fedha (ATM) zaidi ya 800 nchini na mawakala zaidi ya 700. Amesema pia, kwa uwepo wa Soko la Dhahabu Geita wameona ni vyema kusogeza huduma karibu ikiwa ni miongoni mwa njia ya kuthibitisha kuwa NMB ipo bega kwa bega na serikali, huku akiwashukuru wateja kwa kuwa wavumilivu na kuwaomba kutumia vyema huduma zitolewazo na benki hiyo kama vile akaunti ya FANIKIWA kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali kwa kupatiwa mikopo
Richarch ameendelea kueleza kuwa, Benki ya NMB ni mdau mhamasishaji wa ulipaji kodi mbalimbali za serikali ambapo hadi sasa, tayari jumla ya Wilaya 168 zimeunganishwa na mifumo ya kielekroniki ya ulipaji wa kodi za serikali.
,Mkuu wa Wilaya hiyo Martha Mkupasi, akatumia wasaa huo kuwapongeza NMB kwa kuitikia wito aliokuwa amewaomba kuufanyia kazi kwa muda mrefu kwa kutambua uhitaji wa huduma ya Benki hiyo wilayani hapo, hivyo akawasihi wananchi kukopa na kukuza mitaji yao kibiashara.
Tawi hilo linatajwa kama suluhu ya kupunguza umbali kwa wa km 50 kutoka masumbwe kwenda Bukombe, na Km 50 kutoka Masumbwe kwenda Kahama ambapo awali wateja wa NMB walilazimika kuzifuata huduma hizo kwa umbali huo.
Mojawapo ya sifa ya Benki ya NMB ni ile ya kuonesha tumaini kwa kuweka kibao cha kuonesha umbali wa kilomita chache kuingia mijini karibia kila mahali ilipo, kweli NMB KARIBU YAKO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa