Rais Magufuli Azindua Barabara yenye Urefu wa Kilometa 45 ya Uyovu - Bwanga Mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli amezindua barabara ya kiwango cha lami ya Uyovu - Bwanga yenye urefu wa Kilometa 45 yenye thamani ya shilingi bilioni 47.
Amewataka wananchi kuacha vitendo vya kuhujumu miundombinu ya barabara kwa kuacha tabia ya kupitisha mifugo na kutochiamba maeneo ya barabara kwa kuwa vitendo hivyo vinaharibu barabara.
Ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa barabara hiyo ambayo itarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa mizigo kutoka Mkoa wa Geita, Kagera, Mwanza, shinyanga na maeneo mengine ya nchi.
Akiwa katika Eneo la Uyovu Wilayani Bukombe Mheshimiwa magufuli ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Bukombe kwa kumpigia kura nyingi amewataka washirikiane vyema na viongozi wazuri wa Mkoa wa Geita kuanzia Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwa pamoja wanafanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Geita
Ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zinazokuwa kwa kasi kiuchumi, Serikali inatekeleza miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kama uwekezaji katika miundombinu ya reli na barabara pamoja na elimu na afya ambapo katika bajeti ya mwaka 2018 shilingi bilioni 266 zitatumika katika sekta ya afya.
Amesisitza suala la amani kwa wananchi wote ili wapate maendeleo "nitasimamia na kulinda Amani kwa nguvu zangu zote watanzania na viongozi wa dini, siasa tusimame pamoja katika hili kwa kuwa pasipo na amani hakuna maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa