Na Boazi Mazigo- Geita RS
Katika hali ya kufurahisha, Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa Geita imeeleza kuridhishwa kwake na uboreshwaji wa huduma kwa jamii hususan afya baada ya kupata shuhuda kutoka kwa wananchi.
Hayo yamejiri Agosti 24, 2023 baada ya kamati hiyo kufanya ziara na kujionea utoaji wa huduma kwenye kituo cha afya Katende wilayani chato ambacho hapo awali ilikuwa ni zahanati tangu mwaka 1975 hadi mwaka 2021. Ilipopandishwa hadhi.
Akiongea kwa wakati tofauti, mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Nicholaus Kasendamila alisema," waliosema huduma ni nzuri ni wananchi, hivyo sisi tumpongeze Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotupa faraja kuboresha huduma. Lakini pia ajira ziliongezeka kutokana na kupanuliwa kwa huduma na kwa kuboreshwa, wananchi wamepata huduma bora"
Mwenyekiti Kasendamila aliongeza kuwa, ni vyema wahudumu na watumishi kwa ujumla kuendelea kuwatia moyo, kuwahudumia wananchi na kudumisha mahusiano, Upendo na mshikamano na kwamba miradi ya serikali inapokuja ni vyema kupokelewa na kusemewa kwa wananchi.
Kwa upande wake Mganga mkuu halmashauri ya wilaya Chato Dkt. Eugen Rutaisire alisema, "kwa sasa hali ya upatikanaji wa dawa ni asilimia 93 na wakazi wa Katende wanaishukuru sana serikali kwa huduma nzuri inayotolewa na kuahidi mbele ya kamati hiyo kuendelea kutoa huduma stahiki kwa Wananchi"
Vilevile Mwenyekiti wa Kijiji cha Katende Bw.Nzoka Butigu aliihakikishia kamati hiyo kuwa huduma zipatikanazo kituoni hapo ni nzuri na zinawaridhisha kisha kuishukuru serikali.
Pamoja na mradi huo, kamati ilipita na kutembelea miradi inayotekelezwa wilayani hapo ambapo gharama yake yote ni zaidi ya shs. Bilioni 42.3
Kamati hii itaendelea na ziara yake Agosti 25, 2023 katika wilaya ya Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa