Na Boazi Mazigo-Geita RS
Geita umekuwa miongoni mwa mikoa iliyoadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa ambayo hufanyika kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka ambapo mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martine Shigela ametumia nafasi hiyo kuongoza wakazi wa mkoa huu kuwakumbuka mashujaa mbalimbali wa Tanzania wakiwemo kutoka Geita na kuwapongeza mashujaa wengine ambao hawatokani na jeshi, lakini pia kuipongeza serikali na watanzania wote kuendelea kuienzi misingi ya kuwakukmbuka wapiganaji wa nchi hii kwani wametoa uhai wao kwa ajili ya wengine.
Ameyasema hayo Julai 25, 2023 katika uwanja wa Mashujaa uliopo mjini Geita baada ya kushiriki zoezi la usafi na upandaji miti eneo la uwanja wa mashujaa na kumpongeza Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa miongoni mwa Mashujaa wa Dunia na Tanzania kutokana na namna anavyoliongoza Taifa licha ya kupokea kijiti cha uongozi baada ya kumpoteza aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano.
“tukiwa tumekusanyika hapa kwa ajili ya kuwakumbuka mashujaa wetu, tambueni yakuwa, Mhe.Rais Samia ni miongoni mwa Marais Shujaa duniani na ndiyo maana tunaendelea kusonga mbele. Sisi wanageita tunajivunia kuwa na mashujaa wengine pia ambao ni waokozi wa afya za watu yani madaktari, wauguzi, walinzi wa Amani (askari), waalimu ambao hutupa wataalam ikiwa tu hutimiza majukumu yao ipasavyo”. Alisema RC Shigela kisha kuiagiza halmashauri ya mji Geita kuhakikisha inalitunza eneo hilo la mashujaa na kulifanyia usafi ili liwe katika hali nzuri
RC Shigela aliongeza kuwa, “ni vyema kila mmoja ajitoe kwa taifa lake ili tuendelee kusonga mbele na tuitumie siku hii kuwaombea dua mashujaa waliotangulia mbele za haki na kwa wale ambao bado wako hai, tuwaombee afya njema”
Kwa upande wake Katibu tawala mkoa Geita Prof.Godius Kahyarara kwa alisema, “siku ya leo itumike kuwakumbuka wenzetu walipigana kwa ajili ya wengine na kuendeleza utamaduni huo”
Naye Manjale Magambo ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa kwaniaba ya CCM alisema, “kwaniaba ya CCM niseme, huwezi kuitenganisha siku hii na CCM kwakuwa ukombozi wa nchi hii unahusiana na chama hiki. Tumetoka kwenye vita na kupigania uhuru, lakini chini ya jemedari Mhe.Rais Samia sasa tunapigania ukombozi wa kiuchumi”
Shughuli hii ilihitimishwa kwa dua na sala kwa viongozi wa dini na ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakuu wa taasisi za umma na binafsi bila kusahau vijana wa jeshi la akiba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa