Na Boazi Mazigo, Geita RS
Katika mwendelezo wa ziara yake kutembelea miradi na kuongea na watumishi, Katibu tawala mkoa Geita Bw.Mohamed Gombati amekutana na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya mbogwe ili kuwa na mwelekeo wa utekelezaji majukumu ya serikali
Akizungumza wakati akihitimisha kikao chake akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Novemba 23, 2023 Bw.Gombati alisema, ni muhimu watumishi kuzingatia nidhamu na maadili katika utendaji wa kazi.
"ninawashukuru kwa michango na maoni yenu, ni vyema niwakumbushe kufanya mambo nane yafuatayo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora, kuwa watiifu kwa serikali, kuwa na bidii ya kazi, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria pamoja na matumizi sahihi ya taarifa kama mtumishi", alisema bw.Gombati.
Alimaliza kwa kusisitiza juu ya viongozi kuanzia ngazi ya kijiji kuhakikisha wanasoma taarifa ya mapato na matumizi, maafisa kilimo kuhakikisha wanatimiza lengo la uzalishaji zao la pamba litakaloiwezesha Halmashauri kufikia tani milioni 20 ndani ya miaka miwili, kukusanya mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuiwezesha Halmashauri kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi na utekelezaji miradi ya Maendeleo
Kwa upande wake katibu tawala wilaya hiyo dkt.Jacob Rombo aliwakumbusha watumishi hao kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kusimamia miradi na kukusanya mapato.
Mwisho, kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo bw. Gerlad Nyaruga alisema, maelekezo yote yaliyotolewa ahakikisha yanafanyiwa kazi na kwamba wamejipanga kuhakikisha kwakuwa ni msimu wa kilimo wanaimarisha lishe kwa kuhakikisha shule zinakuwa na mashamba ili kuendelea kutoa chakula shuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa