Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ametanganza kuanza kwa kamati maalum aliyoiunda yenye jumla ya wajumbe kumi na mbili (12) itakayosimamia mchakato wa kutathimini hatimaye kulipwa fidia kwa wananchi wa Mitaa ya Katoma na Nyamalembo Mjini Geita, suala lililodumu kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo leo tarehe 12.11.2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa geita alipokutana na viongozi watendaji mbalimbali wa serikali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Geita, Ofisi ya Madini Mkazi Mkoa timu aliyoiunda pamoja na wawakilishi wa Mgodi wa GGM, bila kusahau vyombo vya habari
Mhe. Mhandisi Gabriel ameanza kwa kutoa historia kuwa, “miaka ya 2007 kurudi nyuma, Mgodi wa GGM ulianza shughuli zake ambapo ulikuwa ukitumia milipuko ili kupata miamba yenye dhahabu jambo lilipelekea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamika juu ya kupasukiwa nyumba zao. Hii ilipelekea uongozi na mgodi kushughulikia malalamiko hayo ambapo GGM mwezi Oktoba, 2014 waliwatumia Kampuni iitwayo BICO kuanza kuangalia sababu za mipasuko hiyo. Lakini pia Wizara ya Nishati na Madini wakati huo kwa kutumia kampuni ya GST ilifanya taathmini hivyo kuwa na taarifa kutoka pande mbili. Baada ya kuonekana changamoto, watafiti wawili hawa BICO na GST walikuja na kuwa na tafiti moja ambayo ilipelekea kuja na maeneo yanayofanana ikiwemo kushabiliana kwa taarifa za mitetemo yaani wote walithibitisha.
pia Mgodi haukufanya tathmini ya kina walipokuwa wakifanya tathmini ya mazingira, kuangalia nyumba zote na hali za majengo hayo ili kujiridhisha kama nyumba zilikua na nyufa kiasi gani na mwisho majengo kutofautiana mipasuko kulingana na eneo majengo yalipo.
Taarifa hiyo kupitia kipimo cha mitetemo ilionesha kuwepo kwa baadhi ya mitetemo hadi 5.7 ambayo inaleta madhara makubwa”.
Mhandisi Gabriel ameongeza kusema kuwa, mwezi novemba 26, 2018 Mgodi wa GGM ulipewa na serikali siku thelathini (30) kupitia taarifa ya tathmini ya milipuko ya baruti kwa mitaa husika ili kufidia jambo ambalo halikufanyika baada ya muda huo kuisha.
Hivyo, asema yeye kama kiongozi wa serikali ndani ya mkoa, leo tarehe 12.11.2018 anatangaza rasmi kuanza kwa zoezi la tathimini la siku thelathini (30) kwa makazi yote yaliyoathirika na lijikite kwenye maeneo yafuatayo:-
a) Kutambua nyumba zote zilizoathirika zilizo ndani na nje ya bikoni ya Mgodi
b) Kutathmini gharama za uharibifu uliotokea kwa mujibu wa sheria na taratibu katika uthaminishaji mali
c) Gharama zitakazojitokeza, Mgodi utatakiwa kulipa mara moja.
d) Vilevile wananachi wanaoishi mita 900 ndani ya eneo la leseni, na wanatakiwa walipwe fidia watoke kuepuka athari za kimazingira na kiafya.
e) Mgodi pia unatakiwa kutoa taratibu zitakazotumika ili kujiridhisha na kutorudiwa kwa matatizo kama haya kwa wananchi kwani sasa linatakiwa suluhisho la kudumu.
Mwisho, Mhandisi Gabriel akatoa angalizo kwa yeyote atakayejaribu kwa tamaa zake kuvuruga mchakato huu ndani ya kamati aliyoiunda, viongozi wa mtaa na wawakilishi wa wananchi wa maeneo yatakayofidiwa na akasema hatoshindwa kubadilisha mjumbe wakati wowote na kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atakayepanga kuharibu.
Naye Mhe. Leonard Bugomola, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita akashukuru Mhe. Mhandisi Gabriel kwa hatua hiyo iliyofikiwa na kusema kuwa huo ni mwanzo mzuri na anaamini baada ya hapo wananchi wengi watakuwa na amani ya moyo kutokana na kusubiri kwa muda mrefu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa