Huu ni mwendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, na tarehe 12.11.2018 ametembelea vijiji vya Halmshauri ya Wilaya ya Geita katika kata za Nyakamwaga, Bukoli na Nyarugusu, huku akishiriki kuchimba na kujenga misingi ya zahanati akihamasisha kampeni aliyoianzisha ya kupunguza changamoto kwenye sekta ya elimu na afya kwa kuboresha miundombinu ya sekta hizo huku akihimiza azma ya Serikali ya Mkoa ni kumaliza Zahanati kila kijiji kabla au ifikapo juni, 2019
Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhe.Mhandisi Robert Gabriel amezidi kujionea jinsi wananchi walivyoitikia wito wa maendeleo wakihakikisha wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo madarakani.
Baada ya kushiriki uchimbaji wa msingi, Zahanati ya Kijiji cha Bugalahinga Kata ya Nyakamwaga, Mhe.Mhandisi Gabriel amewapongeza sana wananchi wa kijijichi hicho huku akina mama wakisomba mchanga kwa furaha huku watoto wao wakiwa migongoni wamebebwa na kusema “kwa kazi ninayoishuhudia, hii ni dalili kuonesha kuwa, uongozi wa eneo hili kuanzia Mhe. Diwani uko imara na kuna ushirikiano hivyo natamani kuona mama atakayepata ujauzito leo ajifungulie kwenye zahanati hii”. Pia Mhandisi Gabriel amewaasa kumaliza ujenzi wa boma haraka iwezekenavyo ili waweze kupata fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya upauaji. Vilevile amewaomba wananchi wa eneo hilo kujenga nyumba ya mtumishi ili zahanati inapokamilika basi aweze kukaa karibu na kituo kisha akatoa namba yake ya simu ili wananchi waitumie kumpa taarifa mbalimbali.
Kisha Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Geita Mhe. Elisha Lupuga na Kaimu Mkurugenzi Bw. Donald Nsoko wakatoa ahadi ya milioni tano (Tshs. 5,000,000/=) na mifuko hamsini (50) kwa ajili ya saruji ya kufyatulia matofali huku akiwahimiza kumaliza maboma maana . Naye Kaimu Katibu wa CCM Wilaya Bw. Said Kimwaga Said akatoa mifuko kumi (10) kwaniaba ya Chama Tawala Wilaya.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa ulielekea kijiji cha Ikina, Kata ya Bukoli na kushiriki kuchimba msingi wa Zahanati ya kijiji hicho na kuwashukuru wananchi kwa kujitolea akisema “hatutaacha kijiji, ni lazima vyote viwe na Zahanati” huku asisitiza kuwa angependa mama atakayebeba ujauzito siku ya leo basi ajifungulie kwenye zahanati hii.
Mhe. Lupuga kwaniaba ya Halmashauri akaahidi kutoa mifuko hamsini (50) ya saruji pamoja na Tshs.5,000,000/= ili kuunga mkono juhudi za wananchi.
Baada ya hapo, Mkuu wa Mkoa alielekea Kijiji cha Ililika, Kata ya Nyarugusu na kushiriki kujenga msingi wa zahanati ya Ililika uliojengwa kwa nguvu za wananchi kisha akazungumza na wananchi wa kata hiyo akiwasisitiza juu ya kumaliza Zahanati kila kijiji kabla au ifikapo juni, 2019.
Hapa Makamu Katibu wa CCM Wilaya Bw. Kimwaga kwaniaba ya Chama Cha Mapinduzi akaahidi mifuko mitano (5) ya saruji, huku mwenyekiti Lupuga akiahidi mifuko hamsini (50) ya saruji na shilingi milioni tano (Tshs.5,000, 000 ) ili waanze ujenzi wa nyumba ya mtumishi.
Kisha alitembelea na kujionea hatua za ujenzi wa uboreshaji miundombinu Zahanati ya Nyarugusu ambayo baada ya kukamilika miundombinu inayoongezewa itakuwa Kituo cha Afya ambapo pia alilisisitiza matumizi ya “force account” vilevile akawaomba wananchi kupenda kujitolea kushiriki ujenzi wa miradi ya maendeleo na si kutanguliza maslahi mbele.
Mkuu wa mkoa alihitimisha ziara yake kwa kuongea na watumishi wa Halmashauri akiwakumbusha juu ya kuwa na mfumo wa uthibiti vifaa vya ujenzi lakini pia kuwa mradi mkakati utakaoziongezea Halmashauri mapato. Amewaeleza pia juu ya kuwa na maadili na uadilifu kazini huku akionya watumishi ambao bado wana mawazo ya kuiba fedha za miradi.
Kumbuka, kila alipopita aliwasikiliza wananchi na kutoa namba yake ya simu ili wananchi wasaidie kukomesha vitendo viovu kwa kutoa taarifa hizo kwake.
Katika ziara hiyo, walikuwepo pia uongozi wa CCM Wilaya, Kamati ya Fedha na Mipango pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa na wataalam wa halmashauri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa