Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ameendelea kunadi fursa za Mkoa wa Geita alipotembelea banda la Mkoa huu kwenye Maonesho ya 42 Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akiwa kwenye banda hilo, Mhe. Mhandisi Gabriel amewahamasisha wadau wa biashara na wawekezaji kushiriki katika Jukwaa la Biashara la Mkoa wa Geita ambalo litafanyika kuanzia tarehe 15 hadi 16.08.2018 Mkoani Geita pamoja na Maonesho ya Teknolojia ya Uchimbaji wa Madini yatakayofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 29.09.2018.
Aidha, Mhe. Mhandisi Gabriel amefanya hamasa kubwa kwa kupita katika kila banda kwenye maonesho hayo kwa ajili ya kuunadi Mkoa wa Geita kwa wadau mbalimbali, jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine limeongeza tija kwa Mkoa kwa wadau kufahamu mazuri ya Mkoa wa Geita.
Wafanya biashara na wawekezaji mnaalikwa kushiriki kikamilifu wakati wa jukwaa hilo la Biashara la Mkoa muda utakapofika lakini pia katika maonesho ya Teknolojia ya uchimbaji wa Dhahabu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa