Wajasiliamali wadogodogo ni miongoni mwa kundi ambalo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe .Rais Dkt. John Pombe Magufuli imelipa kipaumbele kwa hukikisha wanaepukana na kero zitokanazo na ushuru/tozo mbalimbali na hivyo kuja na vitambulisho kwaajili yao vinavyouzwa shilingi elfu ishirini kwa matumizi ya mwaka mmoja.
Jitihada hizo zinapelekea uongozi wa mkoa huu kupitia Mkuu wa Mkoa Mhe. Mhandisi. Robert Gabriel kufanya ziara ya kushtukiza tarehe 05.03.2019 katika Soko la Lyobaika, Kijiji cha Lyobaika katika kata ya Uyovu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ili kujiridhisha kama wajasiliamali hao wanafanya biashara zao wakiwa na vitambulisho. Baada ya kupita kwa wajasiliamali hao anagundua kuwa, wengi hawakuwa na vitambulisho hivyo akaamua kuitisha kikao cha pamoja ili kuzungumza nao juu ya umuhimu wa vitambulisho hivyo huku akiwahamasisha kuvichangamkia.
Amesema, “tunapenda nyote mpate vitambulisho hivi lengo ikiwa mfanye shughuli zenu bila bugdha yoyote kama lilivyo agizo la Mhe. Rais, lakini mkumbuke kuwa, orodha yenu ni muhimu kuwezesha mipango ya serikali hata katika ujenzi wa masoko".
Baada ya fursa ya maswali na majibu, Mhandisi Gabriel akawapa muda wa hadi tarehe 01.04.2019 kuwa wamemaliza zoezi hilo la kuwa na vitambulisho huku akiwahahakikishia kutotozwa fedha yeyote kwa atakayechukua kitambulisho na kwamba endapo wataombwa fedha baada ya kuwa na utambuzi huo, wasitoe kiasi chochote na atawashughulikia watakaojaribu kufanya hivyo.
Akimaliza kuongea na wananchi hao, Mhandisi Gabriel amewahimiza juu ya matumizi ya Bima ya CHF Iliyoboreshwa ambapo mwananchi ataweza kupata bima hiyo kwa shilingi elfu thelathini huku akitibiwa na wategemezi wake sita, kwamba ni mkombozi wa wao waichangamkie.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba alimtambulisha Mkuu wa Mkoa kwa wajasiliamali na kuwaambia kuwa, kila mjasiliamali ambaye mtaji wake hauzidi milioni nne anao wajibu wa kuwa na kitambulisho hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko hilo, Bw.Gembe Kahindi amewaomba wajasiliamali hao wasiendelee kuweka visingizio ilihali wamepata auheni ya ulipaji ukizingatia zamani walikuwa wakitozwa ushuru mdogo mdogo ambao kwa mwaka ulifikia hadi shilingi elf sabini, lakini kwa sasa ni kidogo, hivyo kuishukuru serikali kwaniaba ya wajasiliamali waliokusanyika hapo, kisha mkutano kufungwa na kuacha walikuwa hawana vitambulisho hivyo wakivichangamkia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa