Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amefanya uzinduzi wa Kampeni inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) uliofanyika tarehe 08.09.2018 katika uwanja wa CCM Kalangalala uliyopo Mjini Geita.
Akiwa Mgeni rasmi, Mhe. Mhandisi Gabriel amewaasa wana Geita na Watanzani kupenda vya nyumbani, hii ikijumuisha huduma za simu kama TTCL, huduma za usafiri kama Air Tanzani hata bidhaa zinazotolewa ndani ya nchi na kwa kufanya hivyo ni dhahiri kuwa tutaujenga uchumi wa Tanzania yetu. Kwa kutambua unafuu wa gharama za mtandao wa TTCL Mkuu wa Mkoa wa Geita ameomba wananchi kujitahudi kuwa wazalendo kwakuwa huduma za makampuni ya Tanzania zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Amesema, “shirika hili ni la kizalendo na ndiyo maana baada ya kupata faida wameirudisha Serikalini, hivyo hata kwako mwananchi, uzalendo ni unapokuwa na laini mbili za simu, moja iwe ya TTCl, ukiwa na laini tatu za simu, moja iwe ya TTCL, na kumbuka unaponunua vocha na vifurushi vya TTCL, fedha hiyo itarudi baadaye kama Gawiwo na mtapata huduma za afya, elimu, barabara n.k”, kisha akafanya uzinduzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Waziri Kindamba amewashukuru wakazi wa Geita kwa kuipokea vizuri kampeni hiyo na kuwaahidi huduma bora zinazokidhi viwango ili kuthibitisha kuwa kweli Nyumbani Kumenoga.
Awali Mkuu wa Mkoa alimpokea Mkurugenzi huyo ofisini kwake na kuzungumza juu ya uwekezaji mkubwa ndani ya mkoa unaohitaji mawasiliano imara kama ya TTCL, lakini pia akawakaribisha TTCL kufungua ofisi kwenye soko jipya la kisasa linalojengwa Mjini Geita akizidi kuwahakikishia watanzania wawekezaji wote kuwa Geita ni mahali salama pa uwekezaji na kama serikali wao watahakikisha mazingira mazuri yanaandaliwa.
Katika kuusindikiza uzinduzi huo, wakazi wa Geita walipata burudani kutoka kwa wasanii maarufu nchini yaani Aslay na Shilole (Shishi Baby)
Ewe mwana Geita na Mtanzania, unasubiri nini kuwa mzalendo kwa Taifa lako?. Hakikisha uakuwa na laini ya TTCL na unatumia vifurushi vyake kwa kuwa ni vya bei nafuu sana na mtandao una kasi.
Vilevile Mkuu wa Mkoa wa Geita anawaalika kushiriki Maonesho ya Teknolojia ya Dhahabu yatakayofanyika Mjini Geita kuanzia tarehe 24-30/09/2018 katika uwanja wa CCM kalangalala. Haya si ya kukosa kwani wachimbaji na wafanyabiashara ya dhahabu watakutanishwa na makampuni na taasisi mbalimbali ili kuweza kuwainua katika uchimbaji wenye tija lakini pia watoa huduma wote waliyopo kwenye mnyororo wa thamani wa Madini ya Dhahabu.
“Rudi Nyumbani Kumenoga”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa