Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigela ametoa wito kwa walimu wote ndani ya Mkoa wa Geita kutumia huduma zinazotolewa na Benki ya NMB.
Mhe. Shigela ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua Kongamano la Walimu Spesho lililoandaliwa na Benki ya NMB Julai 14,2025 Katika Ukumbi wa Mikutano wa Otonde Manispaa ya Geita.
Mhe.Martine Shigela amesema kuwa NMB ni Benki yenye masharti nafuu kwa utoaji wa mikopo kwa walimu na wateja wao wengine Mkoani Geita. Aidha watumie fursa ya kongamano lililoandaliwa kwani litawasaidia walimu kupata mikopo kwa masharti nafuu ,kupata elimu ya utunzaji wa fedha na kujua fursa za biashara zilizopo mkoani Geita.
"Program ya mwalimu spesho imetupa mikopo kwa masharti rafiki mpaka walimu wamejenga nyumba za kuishi kwa kigezo cha hati ya kiwanja,pili unapata elimu ya kutunza fedha na inafundisha fursa za kibiashara"ameongeza Mhe.Shigela
Mkuu wa Mkoa wa Geita amewasisitiza walimu wanaofanya biashara kupata elimu kupitia Program hii ya Mwalimu spesho ili kujitoa kwenye janga la umasikini na magonjwa mkoani Geita.
Aidha ameipongeza benki ya NMB kwa kuboresha huduma za kibenki kidigitali ambazo zinamfanya mtumiaji aweze kupata huduma ya kutoa na kutuma pesa wakati wowote na mahali popote pindi akijiunga na mtandao wa kibenki (Internet bank).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Ndg.Yefred Myenzi ameipongeza benki ya NMB kwa kuboresha huduma za fedha kwa kuangalia walimu ambao ni kiungo kikubwa katika jamii.
Aidha amewasisitiza NMB benki kuwa kipaumbele kuhakikisha wanaikumbuka jamii kwa kutoa madawati mashuleni, vifaa tiba kwenye vituo vya afya pamoja na kuhamasisha watumishi wa umma na wafanyabiashara kutumia huduma ya kidigitali ya Internet bank.
Kwa Upande Wake Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Bi.Faraja Ng'ingo,amesema Kongamano hili linatimiza miaka 10, lengo mahususi ni kuwahudumia walimu, kukutana na walimu kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu akaunti maalum ya vikundi,maboresho ya mikopo ya "Mshiko fasta"ya kukopa kidigitali mpaka shilingi Milioni kumi.
Aidha ameongeza kuwa Kongamano hili limelenga kutoa elimu kuhusu ujasiriamali,kilimo,biashara,elimu ya fedha,teknolojia,ustaafu na afya.
Kongamano hilo limefanyika Nchi nzima likiongozwa na kauli mbiu isemayo"Mwalimu Spesho,Ushiriki Endelevu Wenye Tija"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa