Na Boazi Mazigo-Geita.
Mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martin Shigela Agosti 22,2022 amekutana na kufanya kikao na makundi maalum ya wazee pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wa mkoa wa Geita ambapo ameahidi kutumia uzoefu na maarifa ya wazee na viongozi hao katika utekelezaji wa masuala mbalimbali akikumbusha kwamba hata baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Nyerere aliwatumia wazee na viongozi wa dini wakati akipambana kuutafuta Uhuru wa nchi hii.
Akiongea wakati wa kufungua na kuaihirisha kikao hicho, Mhe.Shigela amesema anamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuitumikia Geita na kwa dhamira aliyo nayo ya kubadili Geita hata kuinganisha na mikoa ya Mwanza na Shinyanga kupitia miundombinu ya daraja na barabara za lami akisema ni hekima ndizo zimewaongoza kukutana makundi hayo muhimu na kujifunza kutoka kwao, hivyo kusisitiza masuala muhimu matatu katika kuleta mafanikio.
Amesema, “unapokuwa mgeni mahali fulani, ni vyema kukutana na wazee. tutatumia uzoefu, ushauri na maarifa yenu kwani hata aifa letu ni salama kwa sababu ya mchango wenu msingi mliouweka, hivyo sisi hatutabomoa misingi hiyo. Mkoa wetu una mambo mengi mazuri, hivyo tukiimba wimbo mmoja pamoja na nyie, itatusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo”.
Vilevile Mhe.Shigela amemaliza kwa kusisitiza juu ya kudumisha amani, umoja na mshikamano na kwamba watu wanapopendana wataishi kama ndugu hivyo ushirikiano ni muhimu pia kisha kusisitiza juu ya viongozi hao kuhimiza makundi wanayoyaongoza kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi la Agosti 23, 2022.
Katika kikao hicho, mwenyekiti wa CCM mkoa Geita Alhaj Said Kalidushi amemweleza mkuu wa mkoa kuwa, mkoa huo unaendelea vizuri na viongozi wana ushirikiano ikiwemo Kamati ya Usalama Mkoa na kusema kuwa anaamini makundi hayo yatatoa ushirikiano huku akishukuru kwa mkoa wa Geita kumpata katibu tawala mkoa mwenye ujuzi na masuala ya uchumi na uwekezaji.
Mwisho, katibu tawala mkoa Prof.Godius Kahyarara ametumia fursa hiyo kujitambulisha kwa makundi hayo akiahidi kufanya kazi kwa ushirikiano.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa