Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Senyamule amewataka watendaji wa serikali ndani mkoa huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kasi na kwa ufanisi lengo ikiwa ni kumaliza miradi yote inayoletewa fedha nyingi na serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Hayo yameelezwa leo januari 20, 2022 na mkuu wa mkoa huyo wakati akifungua na kufunga kikao kazi kilichoandaliwa kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya mkoa juu ya kuimarisha miradi ya Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari Nchini (SEQUIP) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa kilichowahusisha watendaji wa halmashauri kuweka huku akisisitiza mambo kadhaa ikiwemo kuhimiza wazazi kupeleka watoto shuleni, ukusanyaji wa mapato, usafi wa mazingira na mengineyo
“kwanza tuendelee kumshukuru mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kuzitoa Geita na niwapongeze kwa utekelezaji wa ujenzi wa madarasa ambao tumeshiriki kutekeleza kwa kasi na kufanikisha wanafunzi kuanza shule kwa pamoja, lakini pia niwahimize juu ya kwenda mchakamchaka kwenye utekelezaji miradi mingine tuliyonayo, tuhimize wazazi kuwapeleka watoto shule, tukusanye mapato, tufanye usafi kwenye miji yetu lakini tujitahidi tusirudie makosa ya nyuma kwenye utekelezaji miradi inayokuja” alisema Mhe.Senyamule.
Kabla ya ufunguzi wa kikao hicho cha kuweka mikakati, katibu tawala mkoa wa geita Bw.Musa Chogero alisema, kikao hicho kimekuja wakati muafaka hivyobasi ni muhimu kwa watendaji kutambua ya kwamba Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ametoa na anaendelea kutoa fedha nyingi ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, hivyo kuwasihi kutumia fursa hiyo kujipanga kutekeleza maelekezo na maagizo ya kikao hicho.
Nao wajumbe wa kikao hicho ambao pia ni watendaji wa serikali wameshukuru kwa maelekezo na kuahidi kuyatekeleza ili kuleta ufanisi kwa mkoa na taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa