Na Boazi Mazigo-Geita
Ikiwa zimesalia siku 27 kufikia usiku wa tarehe 23 Agosti, 2022, siku ya Sensa ya Watu na Makazi nchini Tanzania, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Geita Mhe.Rosemary Senyamule amekutana na viongozi na wawakilishi wa makundi maalum mkoani humo kwa lengo la kuwapa elimu ikiwa ni sehemu ya kufikisha hamasa ngazi ya chini kupitia wawakilishi ili kuhakikisha wananchi wote wa Mkoa wa Geita wanahesabiwa ili kuliwezesha taifa kupanga mipango yake.
Elimu hiyo imetolewa Julai 27, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Mwl.Nyerere EPZA Bombambili mjini Geita ambapo makundi ya viongozi wa dini, vyama rafiki vya siasa, viongozi wa machinga, bodaboda, Walemavu, kundi la mama Samia, n.k kwa pamoja wamhemihimizwa kutokuwaacha nyuma walevu kwenye zoezi hilo muhimu.
Akiongea wakati akifunga kikao hicho, Mhe.Senyamule amesema “sensa si jambo la mzaha, ni maisha ya watu, hivyo shime niwaombe viongozi na wawakilishi wa makundi mbambali ndani ya jamii, tumieni vikao, makanisa na misikiti waelezeni waumini na wananchi kushiriki zoezi hili muhimu, sense itafanya Geita ijulikane kimataifa”
RC Senyamule ameongeza kwa kusema, “tunaishukuru serikali inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Geita utakaowanufaisha wakazi wa Geita kwa miaka 30 na kupunguza changomoto iliyokuwepo, jambo ambalo limetokana na takwimu za nyuma, hivyo tunapohesabiwa tutajua mahitaji halisi”
“Nimalize kwa kuwakaribisha kushiriki mwaka mmoja wa hospitali ya rufaa ya kanda Chato ambayo inaadhimisha mwaka mmoja wa mafanikio ambapo huduma mbalimbali zinaendelea kutolewa na madaktari bingwa” alimaliza RC Senyamule.
Nao wawakilishi wa makundi maalum ya jamii kwa nyakati tofauti wamesema wapo tayari na kwamba wamepania kuhesabiwa na kuufanya mkoa uwe namba moja
Akiwasilisha mada kusu mamndalizi ya sensa, Ndg,Khalid Msabaha ambaye ni mtakwimu wa Mkoa wa Geita akitokea ofisi ya Takwimu ya Taifa amesema, kutakuwa na maeneo 2,612 ya kuhesabia watu na kutakuwa na makarani 5,204 siku hiyo, hivyo pamoja.
Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa