SERIKALI YAPONGEZA GEITA GOLD MINE KUCHANGIA VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 69 UPANUZI WA GEREZA GEITA
Serikali ya Mkoa wa Geita imeipongeza kampuni ya Uchimbaji wa madini Geita (GGML) kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha na kimarisha miundombinu ya Gereza la Wilaya ya Geita Mkoani humu kwa kuchangia vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 69.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha inajenga miundombinu muhimu katika Gereza la Wilaya ya Geita ili kupunguza msongamano mkubwa uliopo kwa kujenga mabweni mengine ambayo yatatosheleza mahitaji. Hivyo ameipongeza kampuni ya GGML kwa kuunga mkono juhudi hizo na kuwataka wadau wengine wa Mkoa wa Geita kuiga mfao huo kwa kujitolea kuchangia katika masuala mbalimbali ya maendeleo mkoani humu.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa ASP Elly Maiga kaimu Mkuu wa Gereza amesema kuwa gereza la Geita lina uwezo wakuhifadhi wafungwa 197 lakini kuna kipindi linakuwa na wafungwa hadi 600 ambao wanatokana na kufanya uharifu wa aina tofauti hasa mauaji, uvuvi haramu n.k. Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kupanua gereza hilo kwa kujenga mabweni mapya pamoja na miundombinu ya maji na vyoo ili kuepuka mlipuko wa magonjwa. Vifaa vilivyotolewa na GGM ni pamoja na Simenti, tofali, misumali, mabomba, nondo, n.k, Gereza la Wilaya ya Geita lilijengwa 1947
Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kubadili tabia kwa kuacha kutenda vitendo vya uharifu ambavyo vinasababisha wengi wao kuishia katika magereza. Aidha amesema serikali imekwisha tafuta eneo la ekari 500 huko Nyamgogwa Wilaya ya Nyang’hwale kwa ajili ya shughuli za magereza ikiwemo ujenzi wa Gereza la mkoa kilichobaki ni wahusika kuanza utekelezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa