Na Abraham Mwasimali –RS Geita
Wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri zote katika mkoa wa Geita wameagizwa kufanya msako wa watu ambao ni chanzo cha wanafunzi kukatisha masomo yao.
Agizo hilo limetolewa na mwakilishi wa mkuu wa mkoa Geita ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita mhe.Cornel Magembe wakati wa kilele cha maaadhimisho ya juma ya elimu ya watu wazima lililofanyika Oktoba 18, 2023 katika viwanja vya shule ya msingi ludete, mamlaka ya mji mdogo wa katoro.
‘’niwaagize wakuu wa wilaya pamoja na wakurungenzi wa halmashauri, mfanye msako wa kuwabaini watu ambao ni chanzo cha wanafunzi kuacha shule pamoja na wananchi wasiotoa ushirikiano kuhusu elimu ya watu wazima na watakao bainika wachukuliwe hatua za kisheria”’, alisema DC Magembe.
Kwa upande wake afisa elimu wa mkoa wa Geita bw.Anton Mtweve elisema elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi imewasaidia wanafunzi kujua kusoma,kuandika na kuhesabu pamoja na kujua fani mbalimbali za ufundi na ujasiriamali, lakini pia aliwaomba wananchi waachane na dhana potofu kuhusu elimu ya watu wazima na kujitokeza kuwapeleka watoto shuleni.
‘’elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi ipo kwajili ya kuwasaidia wale ambao hawakuweza kupata elimu ya msingi na sekondari ili iwasaidie wajue kusoma, kuhesabu na kuandika; licha ya hivyo, elimu hii inatoa ujuzi mbalimbali wa ujasiriamali ambapo wananchi wana haki ya kuipata ’’aliongeza Bw.Mtweve
Kwa upande wake mwakilishi wa wanufaika wa elimu ya watu wazima witness masumbuko alisema, licha ya kujua kusoma na kuandika pia wamepata elimu ya ufundi wa kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zinawasaidia kujipatia kipato cha kila siku na kuweza kujitegemea kiuchumi tofauti na kipindi ambacho hakuwa na elimu ya watu wazima.
Maadhimisho haya kidunia huadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 1 mpaka 8 ya mwezi wa tisa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa