Ikiwa umetimia mwaka mmoja tangu kuteuliwa na kuapishwa kwake, mkuu wa mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Senyamule amewataka watumishi wa ofisi anayoiongoza kufanya kazi kwa bidii akiwahusia kufanya kazi zote bila kubagua pale wanapopata fursa ya kuzifanya kwani kwa kufanya hivyo itawajengea nafasi nzuri ikiwa wanayo nia na ndoto ya kukua kiutumishi.
Ameyaeleza hayo Mei 20,2022 alipoketi na kuzungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwa lengo la kusikiliza kero, maoni, ushauri na pongezi kwa serikali kama ilivyo utamaduni wake hata kwa wanachi huku akiwataka watumishi hao kutambua thamani ya nafasi na dhamana waliyonayo lakini pia matajario ya mwajiri wao ambaye ni serikali na kusisitiza namna ilivyo na hadhi ya juu miongoni mwa waajili wengi.
“pongezi kwetu kwa kuhamia jengo jipya la ofisi yetu, huu ni ujasiri na tumshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa ofisi za umma ikiwemo hii. Pili napenda mtambue yakuwa, serikali yetu ndiye mwajili aliye bora kuliko wengine kutokana na namna anavyotutendea watumishi. Vilevile niwakumbushe kuwa mabalozi wema wa mema yanayofanywa na serikali kwa kuwa mambo mengi mazuri yamefanyika na tuendelee kuwa waadilifu”. Alisema Mhe.Senyamule.
Alimaliza kwa kuwakumbusha watumishi kupenda kujiendeleza kitaaluma, kuwa wabunifu katika utendaji kazi, kupendana, kushirikiana, na kwamba serikali itaendelea kuwajali na ndiyo maana Mhe.Rais ameongeza mshahara hivyo watambue kuwa serikali inawapenda na inatamani wananchi wake waendelee kuifurahia.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita Ngd.Herman Matemu alimshukuru Mhe.Senyamule kwaniaba ya Watumishi wa ofisi hiyo akiahidi kutekeleza na kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotokana na kikao hicho, kisha kumuomba mkuu wa mkoa aendelee kutoa ushauri wake kila wakati atakapokuwa ameona jambo la kushauri.
Awali, watumishi mbalimbali walitoa maoni, ushauri na pongezi kwa serikali kwa namna inavyoendelea kuwajali watumishi na kumshukuru Mhe.Rais kwa kupandisha mishahara wakisema, "Asante Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan".
Imeandaliwa na:
Boazi Mazigo
Ag.HGCU
Geita RS
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa