Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaagiza Wakurugenzi wote Nchini kuacha tabia ya kukopa Fedha kwa ajili ya kuzitumia Kwa kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao. Ameyasema hayo jana Jioni Mjini Ushirombo wakati akiwasalimia wananchi wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita alipokua akielekea Wilayani Chato.
Awali akiwasalimia wananchi waliomlaki kwenye Mji wa Masumbwe Wilayani Mbogwe Mhe Rais alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anajenga Barabara za Lami kwani zinadumu Muda mrefu.
Aidha, aliwataka viongozi Wilayani Mbogwe kuacha kuwa wapole kwani kwa kufanya hivyo wanachelewesha Maendeleo Wilayani humo, ni lazima wakemee uzembe na Kuhakikisha wanabuni Mambo ya Msingi kwa ajili ya Kuinua Wialaya hiyo. “Simamieni Maendeleo ya Wananchi wenu, nataka Barabara za Lami hapa” alisema JPM.
Akiwa kwenye Mji wa Runzewe alisimama pia kuwasalimia wananchi Lukuki waliokuwa wamejipanga kandonkando ya Barabara kumwona Rais wao na aliwapongeza Wananchi hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kubadilisha Mji wa Runzewe na kutunza Mazingira.
Mhe. Rais alitoa pongezi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya ya Bukombe aliyejitambulisha kwa jina la Afande Kusura kwa kusimamia vizuri Amani ya wananchi wa Wilaya hiyo kwani sasa hali ni shwari sio kama zamani ambap kulikuwepo na Matukio ya Ujambazi na Uvunjifu wa Amani.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alimshukuru Mhe Rais kwa kuwaelekeza kuanzisha Masoko ya Dhahabu Nchini kwani yameleta matunda makubwa kwenye Mapato ya Dhahabu ambapo alisema Mapato yatokanayo na Dhahabu iliyopatikana ndani ya miezi 10 ya Mwaka 2019 Mkoani Geita kutoka kwa wachimbaji wadogo ni Asilimia 51 ya Dhahabu yote iliyopatikana kwa miaka yote Mkoani humo kwani zimepatikana Kilo 2522 zenye Thamani ya Bilioni 237 wakati Mwaka 2016 ni Bilioni 23 pekee zilipatikana.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alimshukuru Mhe Rais kwa kuwaletea Timu ya Mawaziri Wanane aliyoituma kwenda kwenye Hifadhi Wilayani humo ambayo ziara yao ilimaliza Kabisa migogoro ya Wakulima na Sehemu za Malisho kwa Wafugaji kutokana na Mapendekeoz waliyayatoa kwake.
Baadae Mhe. Rais aliwasalimia wananchi wa Kijiji cha Nyakayondwa na aliwataka kutunza Mazingira wanapofanya Shughuli za Kilimo kwenye Pori linalowazunguka kwani wakilitunza na kuwapa Manufaa kwa muda mrefu.
Kwa mapenzi Makubwa kwa Wananchi pamoja na Uchovu wa Safari na Mikutano mingi njiani, Mhe. JPM alisimama tena kwenye kijiji cha Bwanga kuwasalimia Wananchi na aliwasihi wote kuhakikisha Wanachapa kazi ili kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa