Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule Leo Februari 20, 2022 Katika Ukumbi wa GEDECO Uliopo Mjini Geita Amewaongoza Mamia ya Waombolezaji Kutoa Heshima za Mwisho Kwa Miili ya Marehemu Mhandisi Edgar Mungaya na Bw.Magai Mkama, Watumishi wa Wakala wa Barabara za Vijini na Mijini (TARURA) Mkoani Geita Waliofariki kwa Ajali ya Gari Februari 18, 2022 Wilayani Geita.
Akizungumza Kabla ya Kuanza Zoezi la Kutoa Heshima za Mwisho, Mhe. Senyamule Amewaasa Watumishi Kuendelea Kujifunza Uchapakazi na Uadilifu Kama wa Watumishi Hao waliotangulia Mbele ya Haki na Kutoa Wito kwa Madereva Kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani Huku Akiwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Familia Kuendelea Kudumu Katika Imani na Kumtegemea Mungu Wakati Wote Kwani Yeye Ndiye Faraja Tosha.
"Nimesikia Wasifu wa Marehemu Wote. Kupoteza Watendaji Mwenye Ujuzi na Utaalam, ni Uchungu Sana Ukizingatia hata Wahandisi ni Wachache. Sisi Kama Binadamu Tuombe Mungu Atufariji, Tuwe na Tumaini kwa Mungu". Alisema Mhe. Senyamule
"Neno la Biblia Linasema, Japokuwa Amekufa Angali Anaishi. Neno Hili Litupatie Tumaini. Vilevile, Niwaombe TARURA Kama Itawapendeza, Wahandisi Muipe Barabara Hata Moja jina la Mhandisi Edgar ili Kuenzi Mchango Wake". Alimaliza Mhe. Senyamule Kisha Kuwatakia Safari Njema Wanaosafiri Kwenda Kuwapumzisha Marehemu
Akitoa Neno la Faraja Wakati wa Shughuli Hiyo, Askofu wa Kanisa TAG Geita Mchungaji Simon Masunga Alisema, "Ni Vyema Tuliobaki Kuilinda Imani ili Tuumalize Mwendo Salama, Kwakuwa Kifo Hakina Taarifa. Lakini Pia Tuendelee Kukemea Roho Mbaya Ambayo Sasa Inashamiri Geita ya Watu Kujinyonga na Kutupa Watoto"
Awali Akitoa Salam za Rambirambi, Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Musa Chogero Ametoa Pole Kwa Watumishi na Taasisi ya TARURA Kwa Kuondokewa na Watumishi Wawili Kwa Wakati Mmoja Jambo Ambalo Si Jepesi. Vilevile Ametoa Pole kwa Kanisa na Familia Akisistiza Kuwaombea Marehemu Kila Mtu Kwa Imani Yake Ili Waendelee Kupumzika Kwa Amani.
Marehemu Mungaya Ameacha Mjane na Mtoto Mmoja, na Marehemu Magai Ameacha Mjane na Watoto Watano.
Mwili wa Marehemu Mhandisi Edgar Mungaya Umesafirishwa Kueleka Mkoani Arusha na Mwili wa Marehemu Bw.Magai Mukama Umesafirishwa Kuelekea Mkoani Shinyanga Kupitia Runzewe Bukombe Kwa Ajili ya Maziko.
Bwana Ametoa, na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe.
Boazi Mazigo
AFISA HABARI
RS- GEITA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa