Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel amewataka Viongozi wa Wilaya za Geita kulinda misitu iliyopo kwenye maeneo yao ili kurudisha asili ya Mkoa wa Geita kwenye Ukijani wake. Ameyasema hayo mapema leo alipokua akihutubia Wajumbe wa Kikao cha Kumi cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu ya Mkuu wa Mkoa.
Awali aliwapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa maamuzi ya Kuhamia kijiji cha Nzera, kata ya Nzera kuwa Makao makuu ya Halmashauri hiyo kwani kwa kufanya hivyo wanatekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka Halmashauri zote nchini zinazokaa nje ya Eneo lao la kazi kuhamia kwenye Maeneo yao mara moja.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka pia viongozi wa makundi yote ndani ya Mkoa wa Geita kwa nafasi zao wahakikishe wanatumia siku mbili zilizobaki Kuhamasisha kwa nguvu zote ili wananchi waende kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenda kuhamasisha zoezi hilo.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya Umeme Mkoa wa Geita, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Geita Bwana Joachim Ruweta alifafanua kuwa hadi kufikia Disemba 2019 Vijiji vyenye nishati ya Umeme 339 kati ya 474 ambayo ni sawa na asilimia 72 vitapata Umeme na vingine 135 vitapata Umeme kwenye REA awamu ya tatu mzunguko wa pili.
Kuhusu sekta ya madini nao walijipambanua kuwa wameshatoa Leseni za Wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Geita kwa wachimbaji 1408 mpaka sasa.
Daktari wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo alielezea Kuimarika kwa hali ya Upatikanaji wa Dawa na VItendanishi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya Mkoani humo hadi kufikia Asilimia 96 mwezi Disemba 2018 kutoka Asilimia 52 mwaka 2016.
Aidha, DR. Simeo aliwasihi viongozi kufikisha ujumbe kwa wananchi kuwa Kutakua na kampeni ya Chanjo ya Surua Rubela itakayoanza Mkoani hapa tarehe 17 hadi 21 Oktoba na kwamba maandalizi yake yameshakamilika.
Mhandisi Nicas Ligombi, Meneja wa Maji Mkoa alielezea kuwa kutoka Disemba 2018 kuna ongezeko la asilimia Tatu ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Mkoani humo. Na hali hiyo imeboreshwa kutokana na kukamilika kwa Miradi ya maji vijijini kama vile Chankolongo Wilayani Geita, Mnekezi Chato na Visima virefu 27.
Idara ya Uchumi na Uzalishaji walifafanua kuwa Hali ya Uopatikanaji wa Chakula Mkoani ni Toshelevu na kwamba Mkoa unakadiriwa kuwa na ziada ya chakula cha wanga zaidi ya Tani 267,171. Na kwamba kwa sasa bei ya Mahindi ni kati ya Shilingi 18,000 hadi 20,000 kwa debe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa