katika kuufanya mkoa wa geita kuwa na wataalam wenye ujuzi, ubunifu na utendaji wenye matokeo makubwa wakiwemo watumishi wa umma pamoja na vijna wabunifu, mkuu wa mkoa wa geita mhandisi Robert Gabriel amesema ni muda muafaka kuifanya geita kuwa kituo cha teknolojia hapa nchini.
Ameyasema hayo leo oktoba 15, 2020 wakati akizungumza na ujumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Rwekaza Mkandala walipofika mkoani geita.
"mhe.Rais Magufuli ametupa nguvu ya kuthubutu, hivyo tuthubutu na tuanze kwakuwa tunataka geita iwe kituo cha teknolojia ambayo haipo nchini basi tuikaribishe sisi kupitia mashirikiano mazuri tuliyonayo na chuo hiki huria cha Tanzania na tupo tayari kutoa ushirikiano kuwasaidia vijana wabunifu wa teknolojia", asema mhandisi gabriel.
Mhandisi Gabriel ameueleza ujumbe huo kuwa, mkoa unapenda kuwa na wataalam wenye ujuzi wa hali ya juu kupitia mashirikiano mema baina ya ofisi ya mkoa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwakuwa ni chuo chenye msaada katika elimu hapa nchini na kwamba mkoa wa geita.
Kipekee, mhandisi gabriel ametumia fursa hiyo kueleza mipango ya ujenzi wa masoko ya kisasa ya biashara kwenye wilaya zote za mkoa wa geita na kwamba geita ni kinala wa chakula japokuwa imekua ikijipambanua upande dhahabu pekee ikiwa ndiyo utambulisho mkuu, kisha kuutembeza ujumbe huo kwenye soko kuu la madini geita ili kujionea utendaji wake, ambapo kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa sita mchana wafanya biashara zaidi ya tisini (90) tayari walikuwa wamefika sokoni hapo kwaajili ya biashara ya dhahabu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Rwekaza Mkandala amemshukuru mkuu wa mkoa kwa makaribisho lakini pia kwa kuwa kiongozi mwenye maono lakini pia anayetafsiri maono kuwa vitendo.
Amesema, "duniani kote, hakuna mabadiliko bila viongozi wenye maono, hivyo nikupongeze kwakuwa na maono lakini kubwa zaidi kuyageuza kwenda kwenye uhalisia, kitu ambacho kinaonesha matokeo lakini pia uwezo wa kutumia vizuri rasilimali mlizonazo, hivyo niseme hongera sana", kisha kwenda soko kuu la dhahabu kushuhudia kwa kuishika dhahabu ya gramu 75 yenye thamani ya Milioni Sabini na Tano (75,000,000) na kuona jinsi biashara inavyofanyika.
Kabla ya mweyekiti kuongea, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Elifas Bisanda amesema, kama chuo wanatoa shukrani za dhati kwa maono ya mkuu wa mkoa ya kuboresha teknolojia, wataalamu, kufanikisha maonesho ya madini na teknolojia lakini pia ushirikiano baina ya ofisi ya mkoa na chuo hicho akisema, "huwezi kuboresha chuo kabla ya kuboresha waalimu, na vilevile watoto watapata elimu nzuri ikiwa walimu hawajaendelezwa vizuri, hivyo tunashukuru kwa ushirikiano huu utakaoboresha elimu" kisha naye kufurahia jinsi soko kuu la dhahabu linavyofanya kazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa