Wataalam wa Ununuzi na ugavi, TEHAMA, famasia pamoja na waganga wakuu kutoka halmashauri zote za mkoa wa Geita wamepewa wito kuhakikisha mafunzo waliyopewa juu ya utekelezaji mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa taarifa za Mshitiri (Prime Vendor Management Information System) yanazifikia timu zilizopo ngazi ya vituo ili kuleta ufanisi pale mfumo utakapoanza kutumika.
Wito huo umetolewa na mganga mkuu halmashauri ya wilaya Bukombe dkt.Deograsia Mkapa kwaniaba ya mganga mkuu mkoa Geita wakati akiahirisha mafunzo hayo Machi 16, 2023 katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya mji Geita na kuhimiza washiriki kwenda kuanzisha na kusimamia timu ngazi za vituo ili kutokukwamisha matumizi ya mfumo huo pale utakapoanza kufanya kazi.
“kwanza niwapongeze wakufunzi mmetufundisha kwa vitendo, lakini washiriki wenzangu niwapongeze kwa umakini na niombe sasa twendeni tukasimamie uundwaji wa timu ngazi za vituo lakini pia tujipange kufundisha ndani ya muda mfupi kutoka sasa tusichukue mda mrefu ili mfumo huu usijesahaulika”, alisema dkt.Mkapa.
Dkt.Mkapa amemaliza kwa kuiomba OR-TAMISEMI kushughulikia maoni yaliyotolewa na wajumbe katika kuboresha mfumo ili unapoanza angalau mawazo yao yawe yamefanyiwa kazi kwa lengo la kuongeza ufanisi.
Kwa upande wake bw.Amiri Mhando ambaye ni mjumbe wa kitaifa wa kamati ya uratibu ya Prime Vendor System (PVS) alisema, wanaishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia katibu tawala mkoa kwa kufanikisha uendeshaji mafunzo hayo kupitia wakurugenzi kuwaruhusu wataalam hao kuja kupokea mafunzo na maelekezo juu ya mfumo. Ameshauri pia uundwaji wa kamati ufanyike lakini shughuli za matumizi ya mfumo zifate sheria, taratibu na kanuni, hivyo visingizio havitarajiwi kwenye matumizi ya mfumo huu.
Mwisho, bw.Mhando alisema ni muhimu kuzingatia utoaji wa taarifa ngazi ya mkoa pale ambapo washiriki hao watatarajia kutoa mafunzo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa