Yaliyojiri kwenye kikao kazi kati ya TanTrade na viongozi wa Mkoa wa Geita tarehe 7 Novemba, 2018 katika ukumbi wa mkutano wa TanTrade
Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade aliongoza kikao kazi kwa kuwakaribisha viongozi wa Mkoa wa Geita na kusema kuwa, anashukuru uongozi mzima wa Mkoa wa Geita kwa ushirikiano na TanTrade katika kutekeleza majukumu mbalimbali.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Mhandisi Robert Gabriel alitembelea Maonesho ya pili ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania mwaka 2017 na Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara kwa lengo la kuona namna TanTrade inavyoratibu Maonesho na baada ya Ziara hiyo, Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na TanTrade waliweza kuandaa Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia na Uwekezaji katika sekta ya madini Geita-2018
Mkoa wa Geita mbali na madini na uvivi kwenye eneo la kilimo una fursa nyingi katika mazao ya Alizeti, Asali, Mchele na 'Chia Seeds', Pamba n.k
TanTrade kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliweza kuwajengea uwezo wazalishaji 106 wa mafuta ya mbegu ya awengine ikiwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaunganisha wazalishaji kupata masoko endelevu na TanTrade itahakikisha mafuta ya alizeti yanayozalishwa wilaya ya Chato yanapata 'brand' na kupenya masoko ya ndani na pia itahakikisha mazao hayo yanapata masoko ya nje pia
Nae Ndg Denis Bandisa, Katibu Tawala Mkoa wa Geita amesema kuwa wanaishukuru TanTrade kwa kutoa ueledi wao katika kuandaa Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini- 2018 na tayari Mkoa wa Geita umeshaaza maandalizi ya Maonesho ya pili yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019. Ameongeza kusema kuwa, Mkoa wa Geita unaandaa mradi mkubwa wa ujenzi wa Kituo cha Biashara ambapo ndani ya kituo hicho kutakuwa na eneo la Uwanja wa Maonesho na Eneo la Uwekezaji kwaajili ya Viwanda
Aidha Mkoa wa Geita umeiomba TanTrade iweze kuwasaidia kutoa miongozo katika hatua zote za maandalizi ya mradi huu maana ndio taasisi pekee yenye Mamlaka ya Kudhibiti Maonesho nchini
Pia Mhe.Mhandisi Mtemi Msafiri Simeone, Mkuu wa Wilaya ya Chato alisisitiza kwa kusema kuwa Mkoa wa Geita unania ya kuanzisha mapema Mradi huu mkubwa
Kwa upande wake Bw. Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade alihitimisha kwa kusema kuwa “TanTrade itashirikiana na Mkoa wa Geita katika kufanikisha mradi huo na mwaka 2019 itashirikiana na Mkoa wa Geita katika kuratibu Maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini mkoani hapo”
Kikao kazi hicho kilihudhuriwa na Ndg Denis Bandisa-Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Mhe Mhandisi Mtemi Simeone-Mkuu wa Wilaya ya chato, Mhe Josephat Maganga-Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wakurugenzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Geita Mji pamoja na watendaji wengine kutoka Mkoa wa Geita na TanTrade
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano-TanTrade
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa