Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 zimetoa nuru ya matumaini kwa wananchi wa Wilaya ya Nyang’hwale baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Boksi kalavati linalojengwa katika barabara ya kutoka Kharumwa hadi Nyijundu.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la msingi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava amesema kuwa ujenzi wa madaraja mawili katika barabara hiyo utaondoa adha ya usafiri kwa watu na usafirishaji wa mazao na mizigo mingine hususan wakati wa kipindi cha mvua.
Ndg. Mnzava amesema dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wake wanapata urahisi wa huduma za usafiri katika kipindi kizima cha mwaka, ndio sababu ya kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madaraja hayo.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale Mhe. Hussein Kassu ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwakumbuka wananchi ambao kwa takribani miaka 40 wamekuwa wakipata tabu ya kutovuka kutoka upande mmoja hadi mwingine kutokana na kujaa kwa mto Bukungu na kusababisha shughuli za kiuchumi kwa wakulima, wafugaji na shughuli nyingine kukwama.
Ukiwa wilayani Nyang’hwale Mwenge wa Uhuru 2024 umekimbia umbali wa kilomita 137 na kukagua, kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 13 yenye gharama ya shilingi Bilioni tano, ambapo moja ya mradi mkubwa uliozinduliwa ni mradi wa usambazaji umeme katika kitongoji cha Nyamalapa kwa lengo la kuwawezesha wachimbaji wadogo na wa kati wenye viwanda vidogo vinavyojishughulisha na uchenjuaji madini ya dhahabu kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa