Serikali imesema kuwa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita unaojengwa kijiji cha Nyabilezi Wilayani Chato utakapokamilika utafungua fursa nyingi za kiuchumi na kijamii Mkoani humu.
Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika uwanja ndege wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Prof: Makame Mbarawa (Mb) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema uwanja huu utarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka eneo moja kwenda lingine ndani na nje ya nchi. "Tunataka kuona ndege inatoka hapa Geita inasafiri kwenda Songwe, inatoka songwe kwenda Mtwara na kutoka Mtwara hadi Zanzibar."
Amesema uwanja huu pia utafungua fursa za utalii kwakuwa watalii kutoka maeneo mbalimbali watatumia uwanja wa Mkoa wa Geita kuja kuona utalii na pia watu wa Geita watatumia uwanja huu kwenda maeneo mengine kuona shughuli za kitalii. Hata hivyo, Mheshimiwa Mbarawa alisisitiza kuwa ujenzi wa uwanja wa Mkoa wa Geita unatimiza ndoto ya siku nyingi ya kuwa na kiwanja cha ndege cha kisasa ndani ya Mkoa wa Geita.
Uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita unajengwa kwa kuzingatia viwango vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa anga (IYACO) na utakuwa uwanja wa daraja la 4c ambapo ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 100-200 zinaweza kutua.
Awali akisoma taarifa ya uanzishwaji wa mradi huu Mhandisi Patrick Mfugale Mtendaji Mkuu wa wakala wa Barabara nchini (TANROADS) alieleza kuwa uwanja huu unatekelezwa chini ya Mkandarasi Mayanga Construction kwa usimamizi wa Wakala wa barabara Nchini kwa gharama ya tshs bilioni 39.15 ukiwa na run way ya kilometa 3.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa