Viongozi Mkoani Geita Watakiwa kuzingatia uwazi wanapotekeleza Miradi ya Maendeleo
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amewataka viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Geita kuzingatia uwazi na uadilifu wakati wanapotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Mhandisi Robert Gabriel ametoa rai akiwa Wilayani Korogwe alipokwenda na timu ya wataalam wa miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Geita walipokwenda kujifunza namna Wilaya hiyo ilivyofanikiwa kutekeleza miradi mikubwa na midogo kwa kiwango kidogo cha fedha.
Katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameambatana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri lengo likiwa ni kutembelea na kujifunza utekelezaji wa miradi ya elimu, maji, afya na soko la kisasa.
Wakiwa kwenye mradi wa maji Mtonga mheshimiwa Robert Gabriel amewataka Viongozi wenzake watakaporejea katika maeneo yao ya kazi wakati wa utekelezaji wa miradi wahakikishe miradi hiyo inawekwa wazi ili kila mtu ajue mambo yanayoendelea katika miradi hiyo ili kuwa na uwajibikaji na tija katika miradi. " Suala la uwazi ni muhimu sana katika utekelezaji wa Miradi,wataalam wa zamani wanaendelea kutumika basi nasi twende tukawatumie hawa kwa kuwa bado wanaweza kusiadia kutoa mawazo na ujuzi wao".
Mkuu wa mkoa ameongeza kusema kuwa wakati wa uundwaji wa kamati za ujenzi uwanja mpana unatakiwa kuwepo ili kuwezesha wajumbe kupata kamati sahihi.
Mkuu wa Mkoa alisisitiza pia suala la uwekaji wa bendera ya Taifa katika miradi yote ya Serikali inayotekelezwa kwa kuwa utaratibu huo ni kuonyesha uzalendo kwa nchi.
Ujumbe huo umetembelea majengo ya shule ya msingi Kilimani iliyopo kata ya Mtonga ambapo mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Twalibu Mtunguja aliwahasa kuwa wavumilivu na kuonyesha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa miradi ili kuonyesha mafanikio ya hali ya juu amesema Twalibu.
Kwa upande mwingine Mbunge wa Korogwe Mjini Marry Chatanda amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuna haja ya kuonyesha thamani ya miradi na kutambua nguvu za wananchi wanaoshiriki katika ujenzi huo.
Ziara hiyo ya wataalam wa Mkoa wa Geita Wilayani Korogwe imekuja wakati Mkoa wa Geita upo katika kampeni kubwa ya kufanya mageuzi makubwa katika miradi ya elimu, Afya na Maji kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa